Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 May 2013
Monday, May 20, 2013

nadhani huyu ndo beki tatu bora ulaya kwa sasa.


David Alaba ni mchezaji wa soka wa Bayern munich na Austria timu ya taifa,amezaliwa mwaka 1992 kwa mama Mfilipino na baba wa kinigeria.mama yake ni Nurse na baba yake alikuwa DJ na Rapa.

Anauwezo wa kucheza kama beki wa kulia na kushoto na pia,anaweza cheza kama kiungo mkabaji.Jupp Heynches kocha wa Bayern aliamua kumtumia kama BEKI WA KUSHOTO.

Alitamani kuichezea NIGERIA 2007 kwenye kikosi cha chini ya miaka 17 lakini Nigeria walimtosa wakasema,wanahitaji kutumia wachezaji wa ndani.ndipo alipoamua kujiunga na Austria.

Akiwa uwanjani huwa anafanya mambo kuliko hata umri wake.dogo fundi sana.anakaba,anacheza samba na kushambulia.ni moja kati ya mabeki wa kushoto hatari Duniani.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!