Nadhani huyu ni mtu sahihi pale Bavarians kwa sababu kuna upungufu wa winga wa kushoto ambapo yupo Frank Ribery pekee na pia Gotze ni kiungo mshambuliaji ambaye atamsaidia Ton Kroos ambaye naye yuko peke yake.
Mario Gotze kazaliwa 1992 huko ujerumani na kakulia Dortmund tangu akiwa na miaka 8.kaka yake naye kapitia Pale Dortmund na kwa sasa kuna mdogo wake Gotze ambaye yupo pale Dortmund academy under 15 team.
Bayern wamejaza watu wengi sana kulia,Muller,Shaqill na Arjen Roben kitu ambacho naamini,Gaurdiola hato mleta huku Mario Gotze ingawa anapamudu pia.Nadhani atamtumia sana sehemu ya Ton Kroos.
Gustavo,Martinez ni viungo wakabaji huku,Bastain Schweinsteiger akicheza kama kiungo wa kati pekee.
PEP GAURDIOLA KOCHA MPYA WA BAYERN MUNICH
0 comments:
Post a Comment