DORTMUND NI WANAUME
NIONAVYO MIMI DORTMUND NI ZAIDI YA TIMU.
miaka 3 ya nyuma Nuri sahin Alitangazwa kama mchezaji bora wa Bundasliga na Real Madrid wakamkimbilia na kumnunua.Dortmund hawakuyumba na mwaka uliofuata wakachukuwa ubingwa wa Ujerumani.
Msimu wa mwaka jana Shinji Kagawa akawaka sana akiwa na wazee wa nyeusi na Njano,mzee Ferguson pochi ikamuwasha akamnunua.Dortmund hawakuyumba ingawa wamepoteza ubingwa wa Bundasliga,wamefika fainal ya UCL na kuonyesha kandanda safi.
Mario Gotze kawakimbia tena na kujiunga na mahasimu wao The Bavarians na kunauwezekano Mshambuliaji wao hatari LEWANDOWSKI nae akatoweka lakini,mimi naimani Dortmund bado wataendelea kusumbua.
Jurgen Klopp ameijenga timu katika kutegemeana na sio kutegemea mchezaji mmoja,Ndio maana kukosekana kwa Gotze fainal sio sababu ya wao kufungwa.
Nuri Sahini karudi Dortmund kakuta kina Bender na Gundogan ndo wafalme wa dimba.anakula benchi tu.
0 comments:
Post a Comment