Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 March 2015
Tuesday, March 03, 2015

Adam Johnson aachiwa na polisi
Na Florence George

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya soka ya Sunderland Adam Johnson ameachiwa na polisi wa kituo cha Durham ambapo alikuwa akishikiliwa huku akihusiswa kujihusisha kimapenzi na msichana mwenye umri chini ya miaka 16.

Mchezaji huyo alisimamishwa na timu yake hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza siku ya jumatatu mara baada ya kuthibitisha kuwa mchezaji huyo alikuwa amekamatwa na polisi.

Taarifa iliyoka mchana huu kutoka kituo cha polisi cha Durham zinasema kuwa  mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alikamatwa kutokana na kuhisiwa kujihusisha kimapenzi na msichana mwenye umri chini ya miaka 16,na ameachiwa kutoka mikononi mwa polisi lakini uchunguzi zaidi unaendelea.

Johnson alijiunga na Sunderland mwaka 2012 akitokea klabu ya Manchester City na ambapo akiwa na matajiri hao wa jiji la Manchester alifanikiwa kubeba kombe moja la ligi pamoja na kombe la moja la FA.

Hata hivyo mchezaji huyo hatokuwepo katika kikosi cha Sunderland ambacho kimesafiri kuwafuata Hull City ambapo timu hizo zinatarajiwa kupambana usiku wa leo katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!