Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 March 2015
Tuesday, March 03, 2015

Shujaa aliyeipa Ivory Coast Ubingwa wa AFCON 'Astaafu'


Na Florence George


Unamkumbuka goli kipa alizecheza peneti ya mwisho iliyowapa ushindi timu ya taifa ya Ivory coast dhidi ya Ghana kwenye fainali ya kombe la mataifa ya Afrika(AFCON) nchini Guinea ya Ikweta mwaka huu?.

Kama humkumbuki basi anaitwa Boubacar Barry ambaye mechi hiyo ya fainali ndio ilikuwa ya kwanza katika mashindano hayo ya mwaka huu ambapo alifanya kazi ya ziada mara baada ya  kucheza penati mbili za wachezaji wa Ghana baada ya timu hizo kushindwa kufungana ndani ya dakika 120.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa "Facebook" Barry ametangaza rasmi kustaafu kuichezea na timu ya taifa ya Ivory Coast huku akisema kuwa anajisikia amani kuvaa jezi ya timu ya taifa lake.

Barry amefanikiwa kuichezea timu ya taifan ya Ivory Coast mechi 86 huku pia akiwa ameshiriki katika kombe la Dunia mara tatu na timu hiyo ambayo ni miaka ya 2006,2010 na 2014.

Pia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 alikuwa katika timu ya Ivory Coast iliyofungwa kwa penati na timu ya taifa ya Zambia mwaka 2012 katika fainali ya AFCON zilizofanyika nchini Equatorial Guniea na Gabon.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!