Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 February 2015
Sunday, February 01, 2015

Vigogo EPL watamba.


Na Chikoti Cico

Vigogo wa ligi kuu nchini Uingereza timu za Manchester United na Liverpool zimetamba kwenye michezo yao ya jana baada ya timu zote mbili kuibuka na ushindi katika mfululizo wa mechi za ligi kuu nchini Uingereza.
Timu ya Manchester United iliyokuwa inamenyana na Leicester City kwenye uwanja wa Old Trafford iliibuka na ushindi wa magoli 3-1 katika mchezo huo ambao ulikuwa ni kama wa kulipa kisasi kwani katika mchezo wa raundi ya kwanza Leicester waliifunga United magoli 5-3.
Magoli ya United kwenye mchezo huo yalifungwa na Robin van Persie (dk 27), Radamel Falcao (dk 32) na goli la kujifunga la beki wa Leicester Morgan kwenye dakika ya 44 ya mchezo hivyo mpaka kipindi cha kwanza kinaisha United walikuwa wanongoza kwa magoli 3-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa United kucheza pasi nyingi nyuma na pembeni kama njia ya kupoteza wakati lakini pia kumiliki mpira tofauti na mchezo wa kwanza waliofungwa nyumbani kwa Leicester. Kwenye dakika ya 80 ya mchezo Leicester walipata goli la kufutia machozi kupitia kwa Marcin Wasilewski hivyo mpaka mwisho wa mchezo matokeo yalikuwa 3-1.
Kwenye mchezo mwingine wa ligi kuu nchini Uingereza timu ya Liverpool iliibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya West Ham kwenye mchezo uliopigwa nyumbani kwa Liverpool Anfield.
Mchezo huo uliokuwa wa piga nikupige ulishuhudia Alex Song akitumia nguvu dhidi ya wachezaji wa Liverpool hasa Coutinho na Andy Carroll pia akifanya hivyo hivyo dhidi ya mabeki wa Liver lakini mpaka timu zote zinaenda mapumziko hakuna aliyekuwa ameliona lango la mwenzake.
Kipindi cha pili kilianza kwa Liverpool kuliandama lango la West Ham na iliwachukua dakika sita tu toka kuanza kwa kipindi hicho kuandika goli la kwanza kupitia kwa Raheem Sterling aliyepokea pasi kutoka kwa Philippe Coutinho,
Kwenye dakika ya 68 Daniel Sturridge alichukua nafasi ya Lazar Markovic ikiwa ni mchezo wake wa kwanza baada ya kuwa nje kutokana na kuwa majeruhi kwa siku 153 zilizopita, kuingia kwa Sturridge kuliiongezea nguvu safu ya ushambuliaji wa Liverpool na kwenye dakika ya 80 Sturridge aliifungia Liver goli la pili akipokea pasi kutoka kwa Coutinho.
Hivyo hadi mwamuzi wa mchezo huo Andre Marriner akupuliza kipyenga kuashiria kumalzia mchezo Liverpool walitoka vifua mbele na ushindi wa magoli 2-0 na kufikisha alama 38 kwenye msimamo wa ligi.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!