Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 July 2013
Monday, July 01, 2013

MOYES ATAMBULISHA KIKOSI KAZI CHAKE MAN UNITED...MTIHANI UNAOMKABILI SI MCHEZO!


KOCHA David Moyes ametambulisha benchi lake la ufundi katika siku yake ya kwanza rasmi kuanza kazi Manchester United yenye maskani yake Old Trafford.
Moyes ameungana na watu watatu aliokuwa akifanya nao kazi Everton, Kocha Msaidizi, Steve Round, kocha wa kikosi cha kwanza, Jimmy Lumsden na kocha wa makipa, Chris Woods.
 
Wanachukua nafasi za Mike Phelan, Rene Muelensteen - ambaye ameteuliwa kuwa Msaidizi wa kocha Guus Hiddink klabu ya Anzhi Makhachkala - na Eric Steele ambao wote wameondoka katika klabu hiyo kufuatia kustaafu kwa Sir Alex Ferguson mwishoni mwa msimu uliopita.
 
Desk job: David Moyes gets settled in at Manchester United (complete with mouse mat) on his first day at work
Dawati la kazi: David Moyes ameanza kazi rasmi leo Manchester United
David Moyes
David Moyes
Moyes amesema: "Nimefanya kazi na Steve, Chris na Jimmy kwa miaka kadhaa na ninafurahi wameamua kuungana nami katika klabu hii kubwa.
Welcome: Moyes meets members of staff on his first day of work as the club's new manager at Carrington
Karibu: Moyes amekutana na wafanyakazi kadhaa katika siku yake ya kwanza makao makuu ya klabu yake mpya, Carrington
Welcome: Moyes meets members of staff on his first day of work as the club's new manager at Carrington
Here we go: David Moyes arrives at Carrington for his first official day in charge of Manchester United
Hapa tunaenda: David Moyes amewasili Carrington katika siku yake ya kwanza rasmi kazini Manchester United
New manager David Moyes arrives at Man United
Head on: Moyes faces several challenges as he starts his job at United
Anaingia: Moyes anakabiliwa na changamoto kadhaa katika mwanzo wake wa kazi United
Round, mwenye umri wa miaka 42, amefanya kazi na Moyes tangu Julai 2008 wakati Woods amekuwa kocha wa makipa wa Everton tangu 1998. Oktoba 2011 alikuwa kocha wa makipa wa Marekani.
Lumsden, mwenye umri wa miaka 65, amekuwa akifanya kazi na Moyes tangu akiwa Preston North End na tena Goodison Park.
Makamu Mwenyekiti wa United, Ed Woodward amesema: "Nina imani na David na timu yake mpya katika nafasi hii, na pamoja na benchi lake la ufundi la sasa, sasa tunaweza kuanza maandalizi ya msimu mpya ujao,".
Line up: David Moyes poses with assistant manager Steve Round (left) and coach Jimmy Lumsden (right)
Kikosi: David Moyes akiwa katika picha ya pamoja na Kocha Msaidizi, Steve Round (kushoto) na kocha Jimmy Lumsden (kulia)

Moyes sasa anakabiliwa na mambo matatu makubwa, kwanza kutatua sakata la mshambuliaji Wayne Rooney anayetaka kuondoka, kufuatia kutofautiana na kocha aliyemtangulia, Sir Alex Ferguson.
Unhappy: Rooney struggled to hold down a starting place at United last season
Asiye na furaha: Rooney alisotea namba kikosi cha kwanza cha United msimu uliopita
Lakini pia Moyes anakabiliwa na changamoto ya kuboresha safu ya kiungo ya Manchester United kutokana na kiungo wa sasa Michael Carrick kuonekana yupo katika kiwango cha chini na sasa Paul Scholes amestaafu, huku Tom Cleverley na Anderson wakionekana kushindwa kutatua tatizo hilo tu kwa kuandamwa na majeruhi na kushindwa kuwa wachezaji wa uhakika katika kikosi cha kwanza. 
Angalau Darren Fletcher ambaye ni mgonjwa ameonekana kuweza jukumu hilo, wakati Phil Jones anaonekana anafaa zaidi katika beki ya kati kuliko kiungo.
Tom Cleverley
Anderson
Tom Cleverley (kushoto) na Anderson wameshindwa kuwa wachezaji wa uhakika kikosini United
Top target: Thiago Alcantara, pictured with the Euro 2013 trophy, is wanted by United to provide more invention
Anayetakiwa sana: Thiago Alcantara, akiwa na Kombe la Euro 2013 kwa vijana chini ya umri wa miaak 21, anatakiwa na United akaimarishe safu ya kiungo

Lakini pia kuna suala la wachezaji wa kuondoka, nalo pia ni jukumu la Moyes kuamua. Zaidi ya Rooney, kuna wacehzaji wengine kama Nani - ambaye anatakiwa na Monaco na Juventus - na Anderson aliyesainiwa kama chipukizi mwaka 2007, lakini ameshindwa kuwa na maendeleo mazuri. 
Katika ulinzi, Patrice Evra, mwenye miaka 32 sasa, naye anatarajiwa kuhamia Monaco au PSG kufuatia habari za United kutaka kumsajili Leighton Baines. 
Heading out? Patrice Evra could leave United, especially if they sign Everton's Leighton Baines
Ataondoka? Patrice Evra anaweza kuondoka United, hususan wakimsajili Leighton Baines wa Everton

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!