Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 February 2015
Monday, February 02, 2015

Kumbe Henry aliondoka kwa kilio!!!
Na Chikoti CicoMshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal, Thierry Henry ambaye alistaafu kucheza soka mwishoni mwaka mwaka uliopita amedai aliangusha machozi wakati alipoondoka klabuni hapo mwaka 2007 na kuhamia klabu ya Barcelona kwa ada ya pauni milioni 16.

Pia Henry amesema kilichomsukuma kuiacha klabu ya Arsenal na kujiunga na klabu ya Barcelona ni kutokujua hatma ya kocha wa Arsenal Arsene Wenger kipindi hicho, pamoja na kwamba alikuwa anaenda kuwa mshambuliaji chaguo la nne chini ya Pep Guadiola.

“Sikutazamia kundoka Arsenal lakini nilikuwa na miaka 29 na nikiwa na kiwango kizuri, nilifikiri wachezaji wote waliondoka na sikujua kama Arsene (Wenger) atabaki. Haikuwa rahisi na wakati naondoka nililia, sina aibu kusema. Mimi ni mshindani na ilibidi niondoke”.Alisema Henry wakati akihojiwa na beIN Sport.

“Nilipofika huko Barcelona, Guadiola aliniambia kwamba nilkuwa mshambuliaji chaguo la nne na sitakuwa anayeanza. Nilikubaliana na changamoto na nilipigana, na ushindani unakufanya uongeze kiwango chako. Watu wanaongea kuhusu bahati lakini unahitaji kutengeneza bahati yako mwenyewe. Wakati ukifanya kazi unapata tuzo mwishoni”.

Baada ya kustaafu soka Henry mwenye umri wa miaka 37 amejikita na uchambuzi wa soka kwenye studio za televisheni ya Skys Sport na pia ameanza kusomea ukocha kwa beji ya UEFA ngazi B hko nchini Wales.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!