Searching...
Image and video hosting by TinyPic
23 January 2015
Friday, January 23, 2015

Carlo Ancelotti asema 'Asier Illarramendi hauzwi'




  Na Florence George


Klabu ya soka ya Real Madrid ya nchini Hispania imesema kuwa haina mpango wa kumuuza kiungo mkabaji wa timu hiyo Asier Illarramendi katika kipindi hiki cha usajili  Barani Ulaya.


Illarramendi  mwenye umri wa miaka 24 alijiunga na Real Madrid akitokea klabu ya Real Sociedad mwaka 2013 kwa kitita cha shillingi Euro millioni  30 huku akitegemewa kuwa angekuwa mbadala wa Xabi Alonso alieondoka na kujiunga na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich mwanzoni mwa msimu huu.

Japokuwa Alonso ameondoka klabuni hapo lakini mchezaji huyo amekuwa hapati nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza kutokana na uwepo wa wachezaji wengine kama Toni Kroos,Luka Modric,na Sami Khedira.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa Habari kuelekea mechi dhidi ya Cordoba kocha wa Madrid,Carlo Ancelotti amesema kuwa hawana mpango wa kumuuza mchezaji huyo kwani ni muhimu katika timu  japo amekuwa hapati namba na kuanza katika timu hiyo.

Hata hivyo uwepo wa taarifa za kusajiliwa kwa kiungo mkabaji wa Brazil, Lucas Silva zinzonesha kuwa mchezaji huyo hana nafasi katika timu hiyo huku klabu za Arsenal na Athletic Bilbao zinazoonekana kuvutiwa na mchezaji huyo.

Ancelloti pia alisema kuwa Isco hato kuwepo kwenye mchezo wa dhidi ya Cordoba siku ya jumamaosi hivyo Illarramendi au Khedira mmoja wao ataanza katika mchezo huo.

Mpaka sasa Real Madrid ndio wanaongoza ligi wakiwa na pointi 45 na mchezo mmjoa mkononi huku wapinzani wao Fc Barcelona wakiwa nafasi ya pili wakiwa na pointi 44 huku mabinwa watetezi Athletico Madrid wakina nafasi ya tatu wakiwa na pointi 41.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!