Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 January 2015
Wednesday, January 28, 2015

Ronaldo nje mechi mbili.
Na Chikoti CicoMshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo amefungiwa michezo miwili kufuatia kadi nyekundu aliyopewa kwenye mchezo dhidi ya Cordoba baada ya kumpiga kofi Jose Angel Crespo na kumpiga teke Edimar katika mchezo huo ambao Madrid walishinda kwa magoli 2-1.

Kufuatia adhabu hiyo Ronaldo atakosa michezo miwili ya Madrid dhidi ya Real Sociedad utakaochezwa siku ya Jumamosi na mchezo dhidi ya Sevilla utakaochezwa siku tatu baadaye ingawa atakuwepo kwenye mchezo maarufu kama “Madrid derby” dhidi ya wapinzani wao wa jadi klabu ya Atletico Madrid.

Adhabu hiyo ya Ronaldo ambaye alitarajiwa kufungiwa michezo zaidi ya miwili imekuja baada ya taarifa ya mwamuzi wa mchezo huo Alejandro Hernandez kutokuonyesha kama kulikuwa na aina yoyote ya mchezo wa vurugu kutoka kwa Ronaldo kulitokana na kushindwa kuona tukio la kwanza ambalo alimpiga kofi Jose Angel Crespo.

Ripoti ya mwamuzi huyo ilisema “kwenye dakika ya 83 mchezaji Cristiano Ronaldo alitolewa nje kwasababu ifuatayo: kumpiga teke mpinzani wake wakati hana mpira”.

Kadi hiyo nyekundu aliyoonyeshwa Ronaldo ni ya tisa kwenye maisha yake ya soka mpaka sasa huku mpianzani wake Lionel Messi akiwa ameonyeshwa kadi moja tu nyekundu akiwa anaichezea timu ya taifa ya Argentina, ingawa Ronaldo hajamfikia gwiji na kocha wa timu B ya Madrid Zinedine Zidane ambaye alionyeshwa kadi nyekundu 14 kwenye maisha yake yote ya soka.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!