Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 January 2015
Saturday, January 24, 2015

Real Madrid yamsajili kiungo wa Kibrazili.


Na Chikoti Cico

Klabu ya Real Madrid baada ya kumsajili kinda wa miaka 16 Martin Odeegard kutoka nchini Norway siku ya Alhamisi hatimaye imekamilisha usajili wa kiungo mwingine kutoka klabu ya Cruzeiro ya nchini Brazili Lucas Silva.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye amesaini mkataba wa miaka mitano na nusu na mabingwa hao wa Ulaya baada ya kukataa kujiunga na klabya ya Arsenal ambayo ilionyesha nia ya kumsajili amewahi kuichezea timu ya taifa ya Brazili kwa umri wa chini ya miaka 20 na 2.
Taarifa kutoka klabu ya Real Madrid zilisema “Real Madrid na Cruzeiro wamefikia makubaliano kwaajili ya uhamisho wa mchezaji Lucas Silva ambaye amesaini kwaajili ya klabu mpaka Juni 30, 2020”.
“Mchezaji atatambulishwa Jumatatu Januari 26 saa 7 mchana Santiago Bernabeu baada ya kufanyiwa vipimo vya afya. Baadaye Lucas Silva ataenda maeneo ya Bernabeu akiwa na jezi ya Real Madrid na kukutana na vyombo vya habari kwenye chumba cha habari”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!