Searching...
Image and video hosting by TinyPic
23 January 2015
Friday, January 23, 2015

Van Gaal alalama United ikitoka sare FA.


Na Chikoti Cico

Kocha wa Manchester United Louis van Gaal abaki akilalamikia kila kitu baada ya mchezo wa kombe la FA dhidi ya Cambridge ulioisha kwa sare ya bila kufungana, katika mchezo huo ambao ulipigwa kwenye uwanja wa Abbey Stadium, Manchester United walipewa nafasi kubwa ya kushinda hasa kutokana na kuwa na kikosi imara kuliko timu ya Cambridge ambayo inashiriki ligi daraja la pili nchini Uingereza.
Cambridge ambao walitoka uwanjani wakifurahia matokeo hayo kutokana na kwamba watacheza mchezo wa marudiano kwenye uwanja wa Old Trafford walionyesha mchezo mzuri huku wakiwa na nidhamu kubwa ya kukaba dhidi ya wachezaji kama Radamel Falcao, Angel di Maria na Robin van Persie.
Kocha wa Manchester United huku akionyesha kughadhabika na matokeo hayo akiongea na waandishi wa habari baada ya mchezo huo alisema “kila jambo katika mchezo huu kilikuwa kinyume na sisi, nini namaanisha? Tulitakiwa kuja hapa, uwanja sio mzuri hivyo inaweza kushinikiza namna ya unavyocheza, wapinzani kila mara hucheza zaidi ya ambavyo huwa wanacheza na kuzuia daima ni rahisi kuliko kushambulia”.
Pia kocha huyo hakusita kuwanyooshea kidole wachezaji wake kwa kusema “tulifanya makosa yale yale kama tuliyofanya dhidi ya Yeovil na Queens Park Rangers katika hilo tulicheza katika mufmo ule ule dhidi ya wapinzani na hilo lilikuwa kosa letu”.
“Kipindi cha pili tulicheza vizuri zaidi tulicheza kwa kutulia, hivyo ni huzuni tena kwamba ilibidi tusubiri mpaka mapumziko lakini kipindi cha pili nilifurahishwa, hatukufunga lakini inabidi niwape pongezi Cambridge, walicheza vizuri sana na walikuwa wamejipanga vyema, kwa moyo na walipigana mpaka mwisho”.
“Tungeweza kufunga lakini kwasasa tuna mchezo wa ziada, bado tupo kwenye kombe na hilo ndiyo jambo la muhimu, nimewahi kuona mara nyingi kwamba klabu kubwa wakipoteza mchezo dhidi ya wapinzani wa namna hii”.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!