Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 December 2014
Thursday, December 25, 2014

Asamoah Gyan ndani ya Nyumba



 Na Chikoti Cico

Kocha wa timu ya taifa ya Ghana, Avram Grant atangaza kikosi cha muda mfupi cha wachezaji 31 kuelekea michuano ya Mataifa ya Afrika inayotarajiwa kufanyika nchini Equatorial Guinea kuanzia Januari 17 mwakani. 

Grant amewashangaza mashabiki wa timu hiyo taifa maarufu kama “black stars” kwa kuwaita wachezaji ambao hawajawahi kuichezea timu hiyo ambao ni: 

Enoch Adu Kofi anayeichezea timu ya Malmo ya nchini Sweden, Ibrahim Moro wa AIK Stockholm pia ya Sweden, Daniel Amartey wa FC Copenhagen ya nchini Denmaki na Kwesi Appiah wa Cambridge United ya nchini Uingereza . 

Black Stars wamepangwa kundi C pamoja na Algeria, Afrika Kusini na Senegal. Kikosi kamili: Makipa: Razak Braimah (Mirandes, Spain), Adams Stephen (Aduana Stars), Fatau Dauda (AshGold) and Ernest Sowah (Don Bosco, DR Congo)

Mabeki: Harrison Afful (Esperance, Tunisia), John Boye (Erciyesspor, Turkey), Jonathan Mensah (Evian, France), Jeffery Schlupp (Leicester City, England), Awal Mohammed (Maritzburg, South Africa), Kwabena Adusei (Mpumalanga Black Aces, South Africa).

Wengine ni Baba Rahman (Augsburg, Germany), Gyimah Edwin (Mpumalanga Black Aces, South Africa), Samuel Inkoom (Houston Dynamo, USA), Daniel Amartey, (FC Copenhagen, Denmark) 

Viungo: Rabiu Mohammed (Krasnodar, Russia), Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese, Italy), Afriyie Acquah (Parma, Italy), Solomon Asante (T.P. Mazembe, DR Congo), Christian Atsu (Everton, England), Mubarak Wakaso (Celtic, Scotland).

Wengine ni pamoja na  Andre Ayew (Olympique Marseille, France), Alfred Duncan (Sampdoria, Italy), Albert Adomah (Middlesbrough, England), Frank Acheampong (Anderlecht, Belgium), Adu Kofi (Malmo, Sweden), Ibrahim Moro (AIK Stockholm, Sweden) 

Washambuliaji: Jordan Ayew (Lorient, France), Abdul-Majeed Waris (Trabzonspor, Turkey), Asamoah Gyan (Al Ain, UAE), Kwesi Appiah (Cambridge United, England), David Accam (Chicago Fire, USA).


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!