Mbeya City wakanusha habari zilizotoka leo.
Na Oscar Oscar Jr
Timu ya Mbeya City imetoa taarifa kupitia ukuraha wao wa facebook kuwa, mchezo wao wa ligi kuu kati yao na kagera sugar ambao umepangwa kuchezwa Ugenini January 17, utachezwa kwenye uwanja wa kaitaba, bukoba mkoani kagera na sio CCM Kirumba - Mwanza kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti.
Leo kupitia magazeti mbalimbali kumekuwa na habari za mchezo huo kuhamishiwa kwenye uwanja wa Kirumba mkoani Mwanza kupisha marekebisho ya Uwanja wa Kaitaba kule mkoani Kagera ambao kipindi cha Mvua kama hiki umekuwa na matatizo ya kujaa maji na kufanya mpira kutochezwa vizuri.
Sambamba na habari hiyo, Mbeya City ambayo inakamata nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kucheza mechi nane, wamepanga kucheza mchezo wa kirafiki siku ya Jumamosi tarehe 10 mwezi huu, dhidi ya timu ya Karonga united ya Malawi.
Mchezo huo wa kirafiki utachezwa Wilayani Kyela na siku hiyo jezi zao za msimu huu, zitauzwa uwanjani kwa Sh...20,000 na 17,000 kwa mashabiki walio na kadi za mccfc za benk ya Posta.
Mbeya City ambao msimu uliopita walimaliza kwenye nafasi ya tatu, msimu huu wameanza kwa kusua sua ambapo mpaka sasa wameshinda mechi mbili pekee huku safu yao ya ushambiliaji ikiwa na magoli matatu tu.
0 comments:
Post a Comment