Searching...
Image and video hosting by TinyPic
5 January 2015
Monday, January 05, 2015

Barcelona yatikisika!



Na Florence George

Hatimaye mkurugenzi wa ufundi wa Barcelona, Andoni Zubizarreta  na msaidizi wake, Carles Puyol wameamua kuondoka katika nafasi hizo za kuitumikia klabu hiyo ambayo kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ikinufaika na vipaji vinavyotokana na Akademi yao maarufu kwa jina la La Masia. 

Andoni Zubizarreta alijiunga na klabu ya Barcelona mwaka 2010 wakati timu hiyo iko chini ya Rais, Sandro Rosell na kwa mantiki hiyo ameweza kudumu na klabu hiyo kwa muda wa miaka minne.

Uamuzi huo umetangazwa na klabu ya Barcelona ikiwa ni siku chache tu tangu klabu hiyo ilipofungiwa kufanya usajili kutokana na kusajili vijana wa kigeni kinyume na taratibu.

Watu wengi walidhani baada ya nafasi hiyo kuwa wazi, Carles Puyol ambaye ndiye aliyekuwa msaidizi wa mkurugenzi huyo wa ufundi, angeweza kuchukuwa nafasi hiyo lakini mambo yamekuwa tofauti.

Kupitia ukurasa wa Facebook wa mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona, ametumia muda wake kuwashukuru Uongozi, wachezaji na wanachama wa timu hiyo kwa namna alivyokaa nao kwa umoja na mshikamano huku naye akitangaza kujiondoa kwenye nafasi hiyo.

Puyol amesema sasa ni muda muafaka kwake kwenda kutafuta changamoto nyingine mahali pengine ili baadaye arejee na kulipa fadhila kwa mambo mema ambayo klabu hiyo imemtende. Barcelona ambayo jana ilitoka kufungwa bao 1-0, bado haijatangaza mtu atakayechukua jukumu hilo.








0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!