Searching...
Image and video hosting by TinyPic
17 January 2015
Saturday, January 17, 2015

Gaboni yaendeleza ubabe kwa Burkina Faso




Na Florence George


Timu ya taifa ya Gaboni imefanikiwa kuanza vizuri katika mashindano ya mataifa ya Afrika (AFCON) mara baada ya kuifunga timu ya taifa ya Burkina Faso magoli 2-0 katika mchezo uliochezwa katika dimba ya Estadio De Bata jana Usiku.

Nahodha wa Gabon na ambaye pia ni mchezaji wa klabu ya Borrusia Dortmund ya nchini Ujerumani Pierre-Emerick Aubameyang,ndie aliyekuwa wa kwanza kuifungia timu yake katika dakika ya 16 tu ya mchezo huo.

Burkina Faso walicheza kwa nguvu kutaka kusawazisha goli hilo lakini staa wa timu hiyo Jonathani Pitroipa akionekana kutokuwa makini mara baada ya kukosa magoli katika nafasi mbili zilizoonekana kuwa za wazi.

Katika dakika ya 36 Pitroipa alishindwa kuifungia timu yake huku akiwa amebakia na goli kipa wa Gaboni Dideir Ovono hivyo hadi mapumziko Gaboni walikuwa wanaongoza goli moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Burkina Faso wakishambulia kwa nguvu lakini mabeki wa Gaboni walikuwa makini na kuwazuia washambuliaji wa timu pinzani.

Kipa wa Gaboni alifanya kazi ya nzuri mara baada ya kucheza mpira wa adhabu wa Bertrand Traore dakika ya 64 huku dakika mbili baadae Malick Evoun aliipatia Gaboni goli la pili kwa kichwa na hivyo hadi mwisho wa mchezo,Gaboni ikabeba pointi zote tatu.

 Kwa matokeo hayo vijana hao wa Jorge Costa wanaongoza kundi A wakiwa na pointi 3 huku Equatorial Guinea na  Congo Brazzaville wakifuatia mara baada ya kutoka sare ya goli 1-1 katika mchezo wa Ufunguzi .






0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!