Searching...
Image and video hosting by TinyPic
18 January 2015
Sunday, January 18, 2015

Simba mwendo mdundo!


Na Oscar Oscar Jr

Kocha Goran Kopunovic wa Simba ameonekana kuwa na mwanzo mzuri kwenye klabu hiyo baada ya kuwapatia ubingwa wa Mapinduzi ikiwa ni siku chache tu tangu aliposaini mkataba wa miezi sita na timu hiyo.

Jana wakiwa ugenini mkoani Mtwara kwenye mchezo wa ligi kuu walifanikiwa kupata ushindi wao wa pili wa msimu huu dhidi ya Ndanda Fc ambao wanaonekana kuanza kufanya vizuri siku za hivi karibuni.

Simba ambao wamekuwa wakiandamwa na matokeo ya sare, jana walipata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya vijana wa kocha Abdul Mingange ambao mchezo uliopita walitoka kupata sare dhidi ya timu ya Polis kutoka mkoani Morogoro.

Ushindi huo umewafanya wekundu hao wa Msimbazi sasa kutimiza alama 12 na hii ni ishara kwa timu hiyo imeanza kujivuta kwenye nafasi za juu ambazo zimeshikiliwa na Azam Fc wenye alama17, Mtibwa Sugar ambao wana alama 16 sambamba na Jkt Ruvu.

Simba ambao hapo awali walikuwa wametoka sare michezo sita, kushinda mchezo mmoja na kufungwa mechi moja, jana walipata mabao yake kupitia kwa Danny Sserunkuma ambaye alikuwa akifunga bao lake la kwanza na Elias Maguli aliyepachika bao la pili.

Kocha huyo mpya sasa amekwisha iongoza timu hiyo kwenye mechi sita pasipokupoteza mchezo hata mmoja huku akiibuka na ushindi kwenye mechi tano ndani ya dakika tisini achilia mbali mchezo wake dhidi ya Mtibwa Sugar wa Fainali ya Mapinduzi aliopata ushindi kwa changamoto ya mikwaju ya Penalty.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!