Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 January 2015
Wednesday, January 28, 2015

Fabregas hatihati kuwakosa Man City.

Na Chikoti CicoKiungo wa klabu ya Chelsea Cesc Fabregas anaweza kukosekana kwenye mchezo wa Jumamosi kati ya Chelsea dhidi ya Manchester City utakaopigwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge jijini London.

Kiungo huyo ambaye mpaka sasa amepiga pasi 15 za magoli (assists) katika michezo 22 ya ligi kuu nchini Uingereza atakuwa anapigana na wakati ili kuweza kucheza mchezo huo baada ya kugongana na mchezaji mwenzake wa Chelsea, John Terry kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili ya kombe la Capital One dhidi ya Liverpool jana usiku ambapo Chelsea walishinda kwa goli 1-0 na kuingia fainali.

Febregas alitolewa nje kwenye dakika ya 50 ya mchezo huo na kuelekea moja kwa moja kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwaajili ya matibabu baada ya kuumia mapema mwanzoni mwa kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Ramires .

Pia beki wa kulia wa Chelsea Filipe Luis naye ana hatihati ya kucheza dhidi ya City baada ya kuumia na alitolewa mwishoni mwa kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na David Azpilicueta huku Ivanovic pia akipata majeraha kwenye mguu wakati wa mchezo huo.

“Branislav aliweza kuendelea lakini wengine walishindwa, Filipe Luis alitoka kwa matatizo ya shavu la mguu (Calf) na Fabregas ilitaarifiwa kukaza kwa ukano wa mvungu wa goti. Fabregas alisema alikuwa bado hajaumia lakini ataumia mapema kama akiendelea” alisema Mourinho.

Mourinho aliendelea kusema “sitaki kufikiria kuhusu uchovu, kama tulicheza kwa masaa mawili na kupoteza ningekuwa na wasiwasi zaidi, wanafuraha na wakati ukiwa na furaha unaweza kukabiliana na uchovu lakini ni wazi tulicheza kwa masaa mawili na inabidi tucheze Jumamosi dhidi ya City ambao hawakucheza”.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!