Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 January 2015
Wednesday, January 28, 2015

Arteta aongeza mkataba Arsenal

Na Florence George


Inaki Ibanez amabye ni wakala wa mchezaji wa kimataifa wa Hispania na timu ya soka ya Arsenal, Mikel Arteta amefichua kuwa kiungo huyo ataendelea kukipiga katika timu hiyo hadi msimu ujao baada ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja.

Arteta mwenye umri wa miak 32 alijiunga na washika bunduki hao wa London akitokea klabu ya Everton mwaka 2011 na kusaini mkataba wa miaka minne ambapo mkataba huo ulikuwa unaisha mwishoni mwa msimu huu.

Wakala huyo aliuambia mtandao wa footmercato.net kuwa mteja wake ataendelea kukipiga katika timu hiyo hadi msimu ujao baada ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja hivi karibuni.

Nahodha huyo wa Arsenal amekuwa nje ya uwanja tangu mwezi November ambapo aliumia kifundo cha mguu katika ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Borussia Dortmund katika ligi ya mabingwa ulaya na anatarajiwa kurudi dimbani mwezi April mwaka huu.

Arteta ambaye aliteuliwa kuwa nahodha wa timu hiyo msimu huu baada ya aliyekuwa nahodha wa timu hiyo Thomas Vermaelen kuuzwa kwenda Barcelona na amefanikiwa kucheza michezo saba tu tangu kuanza kwa ligi kuu Uingereza msimu huu. 

 

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!