Searching...
Image and video hosting by TinyPic
22 January 2015
Thursday, January 22, 2015

Congo yang’ara AFCON


Na Chikoti Cico


Timu ya taifa ya Congo yaichapa Gabon kwa goli 1-0 kwenye mchezo wa kundi A wa michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika uliofanyika kwenye uwanja wa Bata nchini Guinea ya Ikweta.

Kwenye mchezo Congo ambao walikuwa kwenye presha kubwa kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara toka kwa Gabon hasa kupitia kwa mshambuliaji wao hatari anayeichezea klabu ya Borrusia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang lakini kwenye dakika ya 48 ya mchezo huo Prince Oniangue aliipatia Congo goli pekee ambalo liliwapa alama zote tatu.

Kutokana na matokeo hayo Congo wanaongoza kundi A wakiwa na alama nne huku Gabon wakishika nafasi ya pili wakiwa na alama tatu na wenyeji Guinea ya Ikweta wakishika nafasi ya tatu wakiwa na alama mbili huku Burkina Faso wakishika mkia wakiwa na alama moja.

Mchezo mwingine wa kundi hilo ulikuwa ni kati ya wenyeji Guinea ya Ikweta dhidi ya Burkina Faso ambao uliisha kwa sare ya bila kufungana na hivyo timu hizo mbili kugawana alama moja moja.

Michezo ya mwisho ya kundi A itawakutanisha Guinea ya Ikweta dhidi ya Gabon huku Congo wakitarajiwa kucheza dhidi ya Burkina Faso.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!