Searching...
Image and video hosting by TinyPic
22 January 2015
Thursday, January 22, 2015

Adebayor azomewa Spurs ikishinda.


Na Chikoti Cico

Mshambuliaji wa klabu ya Tottenharm Hotspur, Emmanuel Adebayor alibaki kuzomewa na mashabiki wa klabu hiyo kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya kombe la Capital One dhidi ya Sheffield United kwenye uwanja wa White Hart Lane ambapo Spurs walishinda kwa goli 1-0.

Mshambuliaji huyo ambaye alipewa unahodha kwenye mchezo huo hakuonyesha mchezo mzuri wa kuwafurahisha mashabiki wa Spurs na wakati anatolewa kwenye dakika ya 65 kumpisha Roberto Soldado mashabiki wa klabu hiyo walibaki kumzomea.

Katika mchezo huo Spurs waliweza kupata goli moja na la ushindi kwenye dakika ya 74 kwa njia ya penati iliyopigwa na Andros Townsend baada ya beki wa Sheffield United Jay McEveley kuushika mpira kwenye eneo la hatari.

Mchezo wa marejeano kati ya timu hizi mbili utachezwa wiki ijayo siku ya Jumatano kwenye uwanja wa Bramall Lane nyumbani kwa Sheffield United na mshindi ataweza kucheza fainali ya kombe la Capital One dhidi ya Chelsea ama Liverpool kwenye uwanja wa Wembley.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!