Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 December 2014
Saturday, December 20, 2014

Salumu Telela anatosha pale Jangwani


Na Samuel Samuel 
0752415551


Miezi 18 toka sasa alimpa tumbo joto sana Athuman IDD " Chuji" . Salum Telela ni mmoja wa viungo bora na wenye uwezo mkubwa wa kumiliki dimba la kati. Mazoezi na uwezo wa Telela haukumshitua Chuji tu bali hata Nadir Canavaro alikaliliwa akisema " huyu ni mrithi sahihi wa Chuji hapo baadae " 

Kikubwa ndani ya kiungo huyo wa chini ni uwezo binafsi wa kumiliki nafasi hiyo na kuwanyima timu pinzani nafasi ya kulitawala eneo la kati. Pia ni fundi wa pasi za kuipeleka timu mbele na si mgeni katika diagonal pass pale timu inapotawanyika kwa ajili ya kumiliki mpira

Majeruhi msimu uliopita yalimfanya mwamba huyo kupotea uwanjani na ndipo alipoibuka Frank Domayo. Cha kushangaza zaidi , Maximo alipotua Yanga alimrudisha fundi huyo kuwa beki ya kulia kama mbadala wa Juma Abdul. 

Lakini mechi ya mtani jembe ilitosha kuwakumbusha wana Dar Young African kwa nini aliitwa " master" . Dakika 30 tu zilitosha kumwambia Maximo " mimi ni kiungo mkabaji kule pembeni hunitendei haki" Huyo ndo Salumu Telela.

Bado Yanga wanaweza kuwa wanahangaika namna ya kuziba pengo lililoachwa na Frank Domayo ambaye alitimkia Azam fc lakini kama kocha ataweka imani kwa Telela, Yanga watakuwa wametatua tatizo la kiungo mkabaji.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!