Searching...
Image and video hosting by TinyPic
17 December 2014
Wednesday, December 17, 2014

Glen Johnson Nje Mwezi Mmoja
Na Florence George

Beki wa klabu ya soka ya Liverpool na timu ya taifa ya Uingereza Glen Johnson anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja mara baada ya kuumia nyonga katika mchezo wa ligi kuu Nchini Uingereza siku ya Jumapili dhidi ya Manchester United.

Mchezaji huyo mwenye umri wa Miaka 30 ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, aliumia nyonga katika kipindi cha kwanza na kushuhudiwa  timu yake ilifungwa magoli 3-0 dhidi ya miamba hiyo ya Old Trafford.

Kwa mujibu wa daktari wa timu hiyo Johnson anatarajiwa kuwa nje kwa mwezi mmoja huku akitarajiwa kufanyiwa vipimo zaidi ilikujua ukubwa wa tatizo na atakosa maandalizi ya timu yake katika kipindi cha Krismasi na mwaka mpya.

Kukosekana kwa mchezaji huyo kutatoa nafasi kwa mchezaji wa kimataifa wa Hispania Javier Manquillo kuziba nafasi yake katika mchezo wa robo fainali siku ya jumatano usiku dhidi Bournemouth katika kombe la Capital One.

 

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!