Searching...
Image and video hosting by TinyPic
18 December 2014
Thursday, December 18, 2014

Hatimaye teknolojia ya goli yabisha hodi Italia





Na Florence George


Baada ya magoli kuwa yanaleta utata kwa sababu ya mwamuzi kutoona kama mpira umevuka mstari au la ,hatimaye teknolojia ya kung'amua goli kama mpira umevuka mstari kutumika msimu ujao katika ligi kuu Nchini Italia maarufu kama Serie A.

Kauli hiyo imetolewa na Raisi wa chama cha mpira wa miguu Nchini humo(FA) Carlo Tavecchio,mara baada ya chama hicho kupigiwa kelele nyingi hatimaye kimekubali mfumo huo kutumika kuanzia msimu ujao.

Teknolojia hiyo itatumiwa katika ligi kuu tu na ianakadiriwa itawagarimu kiasi cha Euro 190,000 huku itakuwa inaboreshwa ili iwezetumika katika ligi daraja la pili Nchini humo.

Klabu ya AC milan itapokea kwa shangwe kubwa habari hizi kutokana na miaka ya hivi karibuni kuwa wahanga wa magoli yao kuwa yanakataliwa na mwamuzi ,  huku yakionekana kuwa yamevuka mstari.

Ungereza ndio iliyokuwa Nchi ya kwanza kutumia mfumo huo katika msimu huu, ambapo pia Ujerumani itautumia msimu ujao, hivyo Italia itakuwa Nchi ya tatu kutoka Barani Ulaya kutumia mfumo huo ambao pia ulitumika katika fainali za kombe la Dunia zilizofanyika Nchini Brazili.




 



0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!