Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 December 2014
Monday, December 01, 2014

Uchambuzi: Manchester United vs Stoke City leo Old Trafford.


Na Chikoti Cico.

Ratiba ya ligi kuu nchini Uingereza inatarajiwa kuendelea tena leo siku ya Jumanne kwenye uwanja wa Old Trafford timu ya Manchester United ikitarajiwa kuikaribisha timu ya Stoke City katika kutafuta alama tatu muhimu.

Manchester United ambao waliibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Hull City kwenye mchezo uliopita na kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi huku wakiwa na alama 22.

Watamkosa kiungo wao mwenye kasi Angel Di Maria aliyeumia kwenye mchezo huo dhidi ya Hull City huku Phil Jones, Luke Shaw, Rafael, Daley Blind na Jonny Evans nao wakiendelea kuwa nje.

Kocha wa United Luis Van Gaal anatarajiwa kuendeleza wimbi la ushindi baada ya kushinda michezo mitatu mfululizo hivyo kuendelea kujikita kati ya timu nne za juu (top four) kwenye msimamo wa ligi huku wakizifukuzia Manchester City na Chelsea kileleni.

Kikosi cha United kinaweza kuwa hivi: De Gea; Valencia, Smalling, Rojo, Young; Carrick, Herrera, Fellaini; Mata; Rooney, Van Persie

Hali si nzuri kwa kocha wa Stoke City Mark Hughes baada ya kupoteza michezo sita mpaka sasa huku timu hiyo ikishika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 15.

Stoke wanatarajiwa kucheza kufa na kupona ili kuondoa wingu baya la kupoteza mechi mfululizo kwa kupata ushindi dhidi ya United hapo Jumanne.

Kuelekea kwenye mchezo huo Stoke watawakosa kiungo Steve Sidwell ambaye atakuwa nje kwa karibu wiki sita na Glenn Whelan ambao wote waliumia kwenye mchezo dhidi ya Liverpool.

Wachezaji hao wataungana na Victor Moses, Robert Huth, Peter Odemwingie na Dionatan Teixeira ambao nao pia ni majeruhi.

Takwimu zinaonyesha Stoke City wamekuwa na rekodi mbaya dhidi ya United ugenini kwani wamefungwa michezo 11 iliyopita katika mashindano yote waliyokutana.

Pia rekodi zinaonyesha kwa ujumla mshambuliaji wa United Robin Van Persie amefunga magoli 10 kati ya mechi tisa alizocheza dhidi ya Stoke City kwenye ligi kuu nchini Uingereza.

Kikosi cha Stoke City kinaweza kuwa hivi: Begovic; Bardsley, Shawcross, Wilson, Pieters; Cameron, N'Zonzi; Walters, Bojan, Diouf; Crouch

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!