Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 December 2014
Saturday, December 20, 2014

Uchambuzi: Manchester City vs Crystal Palace


Na Chikoti Cico

Mchakamchaka wa mechi za ligi nchini Uingereza unatarajiwa kuendelea tena wikiendi hii huku kwenye uwanja wa Etihad timu ya Manchester City ikitarajia kuwakaribisha Crystal Palace katika mchezo ambao kila timu ikihitaji alama tatu muhimu.

Manchester City ambayo inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 36 inatarajiwa kuingia kwenye mchezo kutafuta alama tatu muhimu ili kuendelea kuifukuzia kileleni timu ya Chelsea ambayo inashika nafasi ya kwanza ikiwa na alama 39.

Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini ataingia kwenye mchezo huo huku akiwakosa washambuliaji wake wote Sergio Aguero, Stevan Jovetic na Edin Dzeko ambao wote ni majeruhi na wanatarajiwa kurejea uwanjani mapema mwakani.

Hivyo mshambuliaji mwenye miaka 18, Jose Angel Pozo anaweza kuanza kwenye mchezo huo, pia atamkosa nahodha na beki wake mahiri Vicent Kompany ambaye nae ni majeruhi.

Kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha Manchester City wamekuwa na rekodi nzuri dhidi ya Crystal Palace kwani wameshinda michezo sita iliyopita waliocheza dhidi ya Palace katika mashindano mbalimbali waliyokutana.

Kikosi cha Manchester City kinaweza kuwa hivi: Hart; Sagna, Demichelis, Mangala, Clichy; Toure, Fernando, Nasri, Lampard, Silva; Pozo

Kwa upande wa Crystal Palace hali sio nzuri sana baada ya kucheza michezo minne bila kupata ushindi matokeo yaliyopelekea timu hiyo kushika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 15 hivyo, Palace wanatarajiwa kupigana kufa na kupona ili kupata alama tatu muhimu na kuepuka kushuka chini zaidi kwenye msimamo wa ligi kama watapoteza mchezo huo.

Kocha wa Crystal Palace Neil Warnock ataingia kwenye mchezo huo huku akimkosa mshambuliaji wake Marouane Chamakh na Joe Ledley ambao ni majeruhi lakini Adrian Mariappa ambaye alikuwa ameumia goti kwasasa yuko fiti lakini anaweza asianze kwenye mchezo huo dhidi ya City.

Takwimu zinaonyesha Crystal Palace wamekuwa na rekodi mbaya kwenye mechi za ugenini kwani katika michezo tisa iliyopita ya ligi wameshinda mchezo mmoja tu huku wakifungwa michezo mitatu na kutoka sare michezo mitano.

Kikosi cha Crystal Palace kinaweza kuwa hivi: Speroni, Kelly, Hangeland, Dann, Ward, Jedinak, McArthur, Ledley, Bolasie, Zaha, Gayle

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!