Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 December 2014
Saturday, December 20, 2014

Kumbe Manchester City wamezeeka!!


Na Chikoti Cico

Timu ya Manchester City inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza imeonekana kuwa na wastani mkubwa umri kwa wachezaji wake kwa tafiti zilizotolewa hivi karibuni.

Pamoja na kuwa na mchezaji kama Eliaquim Mangala mwenye umri mdogo wa miaka 23 City wameonekana kuwa na wachezaji wenye wastani wa miaka 28.8 kwenye kikosi kizima cha timu hiyo.

Ndani ya ligi kuu nchini Uingereza City wanaongoza listi ya timu zenye wachezaji “wazee” huku ikifuatiwa na Crystal Palace yenye wachezaji wenye wastani wa miaka (28.4) na Stoke City ikishika nafasi ya tatu kwa wastani wa miaka (28.1).

Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu nchini Uingereza pia wanashika nafasi ya saba kwenye listi ya timu zenye wachezaji wenye wastani mkubwa wa umri barani Ulaya huku timu ya Torpedo Zhodino kutoka Belarus ikiongoza kwa kuwa na wastani wa wachezaji wenye miaka 29.4

Fenerbahce ya Uturuki inashika nafasi ya pili ikiwa na wastani wa miaka 29.3 na Slutsk ya Belarus ikishika nafasi ya tatu ikiwa na wastani wa miaka 29.1.

Ndani ya ligi kuu nchini Uingereza wachezaji wa Manchester City wanaoongoza kwa kuwa na umri mkubwa ni Frank Lampard mwenye miaka (36), Martin Demichelis (33), Yaya Toure (31), Gael Clichy (29), Jesus Navas (29) na Aleksandar Kolarov (29) ambao jumla ya wastani wao peke yao ni miaka 31.2.

Tafiti hizo pia zimeonyesha kuwa ligi kuu nchini Italia maarufu kama SERIA A ndiyo ligi yenye wachezaji wenye wastani mkubwa wa umri barani Ulaya huku ikiwa na wastani wa miaka 27.3 ikifuatiwa na ligi ya nchini Russia yenye wastani wa miaka 27.2 na ligi kuu nchini Cyprus ikishika nafasi ya tatu ikiwa na wastani wa miaka 26.9.

Wakati huo huo tafiti hizo pia zimeonyesha kuwa ligi kuu nchini Uholanzi imejaa vijana zaidi barani Ulaya kwani ina wachezaji wenye wastani wa miaka 24.2 huku timu zinazoshiriki ligi hiyo kama Heerenveen ikiwa na wachezaji wenye wastani wa miaka 22.6 ikifuatiwa na PSV yenye wastani wa miaka 22.8 huku Ajax ikishika nafasi ya tatu ikiwa na wastani wa miaka 23.5

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!