Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 December 2014
Saturday, December 13, 2014

Uchambuzi: Chelsea vs Hull City


Na Chikoti Cico

Ligi kuu nchini Uingereza inatarajiwa kuendelea kushika kasi katika viwanja mbalimbali wikendi hii huku kwenye uwanja wa Stamford Bridge timu ya Chelsea ikiikaribisha timu ya Hull City katika mchezo ambao kila timu itahitaji alamu tatu muhimu.

Chelsea wataingia kwenye mchezo huo huku wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Newcastle kwa magoli 2-1 hivyo wanatarajia kuingia kwa nguvu kutafuta alama tatu muhimu na kuendelea kujikita kileleni huku mpaka sasa wakiwa ana alama 36.

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho ataingia kwenye mchezo huo huku akiwakosa kipa wake namba moja Thibaus Courtois ambaye ameumia mazoezini hivyo Petr Cech atachukua nafasi yake huu ukiwa ni mchezo wake kwanza wa ligi, pia atamkosa kiungo Cesc Fabregas ambaye atakuwa nje akitumikia adhabu ya kadi 5 za njano.

Washambuliaji wa Chelsea Didier Drogba na Loic Remy takwimu zinaonyesha wote wamefunga magoli matatu dhidi ya Hull Cuty katika michezo iliyopita ya ligi.

Kikosi cha Chelsea kinaweza kuwa hivi: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta; Matic, Ramires; Hazard, Oscar, Willian; Costa.

Kwa upande wa Hull City hali yao ni tete zaidi baada ya kuangukia kwenye nafasi ya 18 wakiwa na alama 13 baada ya kutoka sare ya bila kufungana na West Bromwich kwenye mchezo uliopita hivyo wanatarajiwa kupigana kufa na kupona kwenye mchezo huo dhidi ya Chelsea ili kupata alama tatu muhimu.

Kocha wa Hull City Steve Bruce ataweza kumrejesha kikosini nahodha wake Curties Davis ambaye aliachwa nje katika mechi mbili zilizopita huku pia Gaston Ramirez ambaye alikuwa anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu akitarajiwa kuwemo kwenye mchezo huo huku kiungo Hatem Ben Arfa akiendelea kuwekwa nje na kocha huyo.

Kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha Hull City wamekuwa na rekodi mbaya dhidi ya Chelsea kwani hawajawahi kushinda mchezo wowote nyumbani kwa Chelsea huku wakiwa wamefungwa mara 15 na kutoka sare mara tano.

Kikosi cha Hull City kinaweza kuwa hivi: McGregor; Elmohamady, Chester, Dawson, Davies, Robertson; Huddlestone, Livermore, Meyler; Jelavic, Hernandez

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!