Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 December 2014
Thursday, December 25, 2014

Uchambuzi: Burnley vs Liverpool


Na Chikoti Cico

Turf Moor ni moja ya viwanja vitakavyowaka moto siku ya Ijumaa kwenye ligi kuu nchini Uingereza ambapo wenyeji Burnley wataikaribisha Liverpool katika mchezo ambao kila timu inatarajiwa kupigana kwa nguvu zote kutafuta alama tatu muhimu.

Burnley ambayo ilipanda daraja msimu huu wako kwenye hali mbaya na wanaonekana kama watashuka tena daraja kwani mpaka sasa wanashika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 15 huku wakiwa na tofauti ya alama tano na Leicester City wanaoshika mkia.

Burnley inayofundishwa na kocha Sean Dyche kuelekea mchezo huo dhidi ya Liverpool itawakosa beki wa katikati Michael Duff na Stephen Ward ambao ni majeruhi huku Sam Vokes ambaye alikuwa majeruhi akitarajiwa kurejea kikosini kwa mara ya kwanza toka mwezi Machi pia Matt Taylor nae bado anasumbuliwa na majeruhi.

Burnley kuelekea mchezo huo wanaonekana kuwa na rekodi mbovu dhidi ya Liverpool kwani katika michezo minne iliyopita ya ligi waliyocheza nao wameshindwa kufunga goli hata mchezo mmoja pia katika mashindano yote waliyokutana na Liverpool wameshindwa kufunga goli lolote katika michezo mitano kati ya sita iliyopita.

Kikosi cha Burnley kinaweza kuwa hivi: Heaton; Trippier, Shackell, Keane, Mee; Arfield, Marney, Jones, Boyd; Barnes, Ings

Nao Liverpool ambao wanashika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 22 wanatarajiwa kupigana kufa na kupona kushinda mchezo huo ili kujiweka vizuri kwenye msimamo wa ligi na kufufua matumaini ya kurejea “top four”.

Liverpool inayofundishwa na kocha Brendan Rodgers kuelekea mchezo huo itawakosa Fabio Borini aliyepewa kadi nyekundu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Arsenal.

Pia itawakosa Joe Allen, Dejan Lovren, Glen Johnson na Jon Flanagan ambao ni majeruhi. Pamoja na kurejea kikosini Mario Balotelli anatarajiwa kuanzia benchi.

Kuelekea mchezo huo Liverpool wanaonekana kuwa na rekodi nzuri kwa mechi za “Boxing day” kabla ya ujio wa Brendan Rodgers kwani katika michezo 17 iliyopita wameshinda michezo 10 na kufungwa michezo mitano huku wakitoka sare michezo miwili.

Kikosi cha Liverpool kinaweza kuwa hivi: Jones; Toure, Skrtel, Sakho; Lucas, Henderson, Markovic, Coutinho, Gerrard, Lallana; Sterling

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!