Searching...
Image and video hosting by TinyPic
10 December 2014
Wednesday, December 10, 2014

Uchambuzi: Barcelona vs PSG


Na Chikoti Cico.

Moja ya mechi zitakazowakutanisha vigogo kumaliza ungwe ya mwisho ya ligi ya mabingwa Ulaya ni kati ya Barcelona dhidi ya PSG mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Nou Camp.

Mshindi wa mechi hiyo ndiye atakayeongoza kundi F hivyo utakuwa mchezo wa vuta nikuvute katika kutafuta alama tatu muhimu.

Barcelona wanaingia kwenye mchezo huo huku wakishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi F wakiwa na alama 12 hivyo watahitaji alama tatu muhimu ili kuweza kuongoza kundi hilo ingawa tayari timu hiyo kutoka Catalunya imeshavuka hatua ya makundi.

Kocha wa Barcelona Luis Enrique kuelekea mchezo huo atawakosa Dan Alves na Rafinha ambao wamesimamishwa kucheza mchezo huo baada ya wote wawili kuonyeshwa kadi za tatu za njano kwenye mchezo uliopita dhidi ya Apoel.

Kuelekea mchezo huo timu ya Barcelona wameonekana kuwa na takwimu nzuri nyumbani kwani katika mechi 29 zilizopita za ligi ya mabingwa Ulaya wameshinda michezo 22, kutoka sare michezo sita na kufungwa mchezo mmoja tu.

Kikosi cha Barcelona kinaweza kuwa hivi: Ter Stegen; Mathieu, Pique, Mascherano, Alba; Xavi, Busquets, Iniesta; Neymar, Messi, Suarez.

Kwa upande wa PSG ambao wanaongoza kundi F wakiwa na alama 13 wanahitaji kupata sare ya aina yoyote kwenye mchezo huo dhidi ya Barcelona ili kujihakikishia uongozi wa kundi F ingawa tayari nao wameshavuka hatua ya makundi.

Kocha wa PSG Laurent Blanc atamkosa kiungo wake mkabaji Thiago Motta ambaye anasumbuliwa na majeruhi kwenye mchezo huo, wakati huo huo wachezaji wa zamani wa Barcelona Zlatan Ibrahimovic na Maxwell wanatarajiwa kucheza mchezo huo dhidi ya Barcelona.

Timu ya PSG wameonekana pia kuwa na takwimu nzuri kwa mechi za karibuni za ugenini kwenye ligi ya mabingwa Ulaya kwani katika michezo 11 wameshinda michezo saba, kutoka sare michezo miwili na kufungwa michezo miwili.

Kikosi cha PSG kinaweza kuwa hivi: Sirigu; Van der Wiel, Silva, Luiz, Maxwell; Pastore, Matuidi, Verratti; Lavezzi, Ibrahimovic, Cavani

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!