Searching...
Image and video hosting by TinyPic
10 December 2014
Wednesday, December 10, 2014

Uchambuzi: Chelsea vs Sporting Lisbon


Na Chikoti Cico

Ni Chelsea dhidi ya Sporting Lisbon Jumatano ya leo pale Stamford Bridge jijini London Uingereza, hii ikiwa ni moja ya mechi za kundi G katika kukamilisha mechi za mzunguko wa mwisho wa ligi ya mabingwa Ulaya.

Chelsea tayari wameshavuka hatua ya makundi huku wakiongoza kundi G wakiwa na alama 11 katika mechi tano walizocheza hivyo mchezo huo dhidi ya Sporting Lisbon utakuwa ni kwaajili ya kuendeleza rekodi ya kutokufungwa kwenye uwanja wa nyumbani.

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho anatarajia kubadilisha kikosi kwa kutoa nafasi kwa wachezaji ambao wamekuwa hawachezi mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza ili kuwapumzisha wale wa kikosi cha kwanza kwaajili ya ratiba ndefu ya ligi kuu nchini Uingereza.

Kuelekea mchezo huo Jose Mourinho ameonakana kuwa na takwimu nzuri kama meneja dhidi ya Sporting Lisbon huku akiwa hajawahi kufungwa mchezo hata mara moja na timu hiyo toka alipocheza nao akiwa na Benfica, UD Leiria, Porto FC na sasa Chelsea huku akiwa ameshinda michezo mitano na kutoka sare michezo miwili dhidi yao.

Kikosi cha Chelsea kinaweza kuwa hivi: Cech; Ivanovic, Zouma, Terry, Azpilicueta; Ramires, Mikel; Remy, Oscar, Schurrle; Costa

Kwa upande wa Sporting Lisbon mechi hii ina muhimu zaidi kwao kama hawatapoteza mchezo huo dhidi ya Chelsea ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kuvuka hatua ya makundi kwani mpaka sasa wanashika nafasi ya pili wakiwa na alama saba huku Schalke 04 wakishika nafasi ya tatu wakiwa na alama tano.

Kuelekea mchezo huo kocha wa Sporting Lisbon Marco Silva atawakosa kiungo Luis Nani ambaye ni majeruhi na beki Cedric ambaye anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano ndani ya michezo mitano baada ya kuonyeshwa kadi ya tatu kwenye mchezo dhidi ya Maribor.

Kikosi cha Sporting Lisbon kinaweza kuwa hivi: Patricio; Mauricio, Jefferson, Oliveira, Sarr, Carvalho, Mario, Silva, Slimani, Mane, Montero

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!