Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 December 2014
Saturday, December 20, 2014

Suarez afunga goli lake la kwanza ,Barca yapiga mtu 5-0



Na Florence George

Klabu ya soka ya Fc Barcelona ya Nchini Hispania imefanikiwa kufikisha pointi 38 katika michezo 16 iliyocheza msimu huu,pointi moja nyuma ya vinara wa ligi hiyo timu ya soka ya Real Madrid yenye point 39 katika michezo 15 iliyocheza msimu huu ,mara baada ya kuifunga timu ya soka ya Cordoba magoli 5-0 katika mechi iliyopigwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Camp Nou.


Mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania Pedro Rodriguez ambaye katikati ya wiki alifunga Hat trick katika mchezo wa kombe la Mfalme ,ndie aliyekuwa wa kwanza kuifungia Barcelona katika sekunde ya 72 ya mchezo huo akiunganisha mpira uliopigwa na Ivan Rakitic, goli lililo dumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo dakika ya 53 mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay, Luis Suarez aliipatia timu yake goli ya pili huku likiwa goli lake ya kwanza katika ligi hiyo tangu alijiunga na miamba hiyo ya Hispania akitokea timu ya soka ya Liverpool ya Nchini Uingereza.

Cordoba ambao walikuwa wanashambuliua kwa kushitukiza walijikuta wakifungwa goli la tatu na Gerrard Pique akiunganisha  mpira wa adhabu uliopigwa na Xavi, kabla ya nyota wa timu hiyo Lionel Messi kufunga magoli mawili ya haraka haraka na hutitimisha idadi hiyo ya magoli.

Pia katika mchezo huo ilishuhudiwa kiungo mahiri wa Barcelona Xavi Hernandez aliyeingia kipindi cha pili akifikia rekodi ya mkongwe wa Real Madrid Raul ya kucheza michezo 741 akiwa katika klabu moja.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!