Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 December 2014
Saturday, December 20, 2014

Real Madrid Mabingwa wa Dunia






 Na Florence George

Klabu ya soka  ya Real Madrid ya Nchini Hispania imefanikiwa kutwaa kombe la klabu bingwa Dunia, mara baada ya kuifunga timu ya soka ya San Lorenzo ya nchini Argentina magoli 2-0,katika fainali iliyochezwa  siku ya jumamosi usiku huko Nchini Morocco.

Madrid walitawala mchezo huo ambapo katika dakika ya 37, Sergio Ramos aliipatia timu yake goli la kwanza akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Toni Kroos ,goli lililo dumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa Madrid kuendelea kutawala mchezo huo ambapo Mshambuliaji wa kimataifa wa Wales Gareth Bale aliifungia timu yake goli la pili katika dakika 51 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Isco.

Karim Benzema alishindwa kuipatia timu yake goli la tatu baada ya mpira wake kutoka nje sentimita chache kutoka golini,pia usiku huo supastaa wa Madrid Cristiano Ronaldo akishindwa kuunganisha mpira uliopigwa na Benzema katika dakika ya 80,hivyo hadi dakika 90 zinamalizika vijana wa Carlo Ancelotti waliibuka kidedea.

Ushindi huo ulikuwa wa 22 mfululizo msimu huu katika mashindano yote waliyoshiriki,huku wakionekana kuitafuta rekodi iliyowekwa na Ajax ya kushinda michezo 26 mfululizo katika msimu wa mwaka 1971-72.

Kombe hilo ni la nne katika mwaka huu ambapo awali walikuwa wamechukua ubingwa wa klabu bingwa ulaya,kombe la Mfalme,na European Super Cup, huku wakimaliza mwaka huu wakiwa wanaongoza ligi kuu Nchini Hispania pointi moja mbele ya mahasimu wao timu ya soka ya Fc Barcelona.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!