Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 December 2014
Saturday, December 20, 2014

Azam Fc kutupa karata nyingine leo nchini Uganda.


 Na Oscar Oscar Jr

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara, Azam Fc leo hii watashuka dimbani kumenyana na timu ya Vipers Sc ya nchini Uganda katika muendelezo wa ziara yao katika Jiji la Kampala. Azam tayari wameshuka dimbani mara mbili na kujikutaka wakichezea vichapo tu.

Mchezo wa kwanza timu hiyo ilishuka dimbani dhidi ya timu ya SC Villa na mchezo huo ulimalizika kwa mabingwa hao wa Tanzania bara kuchapwa kwa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Nakibuvo jijini Kampala kabla ya kuchezea kichapo tena cha bao 1-0 dhidi ya timu ya Mamlaka ya mapato Uganda maarufu kama URA.

Azam ambao wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania, waliamua kwenda kujificha nchini Uganda ili kupata mechi za kirafiki za kimataifa kwa lengo la kuwapa uzoefu wachezaji wao ambao msimu huu watacheza michuano ya klabu bingwa Afrika kwa mara yao ya kwanza.

Azam Fc wakiwa Uganda tayari wamefanikiwa kumnasa kiungo mshambuliali wa kimataifa wa Uganda na klabu ya KCCA, Brain Majwega na tayari mchezaji huyo amejiunga na wanalamba lamba hao ingawa mchezo uliopita dhidi ya URA hakuweza kuanza kwenye kikosi cha kwanza.

Kikosi kinachoanza leo cha azam ni kama ifuatavyo:
 
1. AISHI MANULA
2. SHOMARI KAPOMBE
3. ERASTO NYONI
4. AGGREY MORIS
5. PASCAL WAWA
6. BOLOU MICHAEL
7. HIMIDI MAO
8. MUDATHIR YAHYA
9. DIDIER KAVUMBAGU
10. SALUM ABUBAKAR
11. KIPRE TCHETCHE
AKIBA
1. MWADINI ALI
2. ABDALLAH KHERI
3. GADIEL MICHAEL
4. DAVID MWANTIKA
5. AMRI KIEMBA
6. BRIAN MAJWEGA
7. KHAMISI MCHA
8. KELVIN FRIDAY
9. WAZIRI SALUM
10. FARID MUSSA
11. GAUDENCE MWAIKIMBA

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!