Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 April 2014
Tuesday, April 01, 2014

WACHEZAJI 10 KUTEMWA NA CHELSEA MWISHO WA MSIMU HUU.

 


Vyombo vya habari nchini Uingereza vimenedelea kuripoti kuwa,kocha wa Chelsea, Jose Mourinho anajiandaa kuwaonyesha mlango wa kutokea wachezaji wawili raia wa Nigeria, John Obi Mikel na Victor Moses. 

Mikel amecheza mara 26 tu kwenye ligi msimu huu lakini,ameendelea kukutana na wakati mgumu sana kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Mreno Jose Mourinho kufuatia ujio wa kiungo wa Serbia, Nemanja Matic aliyejiunga na klabu hiyo ya London dirisha dogo Januari. 

Moses alipelekwa kwa mkopo Liverpool na amekuwa pia sio chaguo la kocha Brendan Rodgers huku,kiungo na winga Raheem Sterling na Phillipe Coutinho wakiwa katika ubora wao na kufanya uwezekano wa Mnigeria huyo kutua kwenye kikosi cha kwanza,kuwa ni ndoto. 

Gazeti kutoka nchini Uingereza la, The Standard,limeendelea kutiirika kuwa,klabu ya Chelsea inampango wa kuachana na wachezaji wake 10 huku majina ya  Mikel, Moses, Fernando Torres na Ashley Cole yakiwa miongoni. 

Mourinho aliweza kuyasema hayo kufuatia kichapo cha jumapili cha  1-0 mbele ya Crystal Palace.kwamba,mabadiliko makubwa ni lazima yafanyike ili kutengeneza kikosi cha ushindani msimu ujao.

Mashaka yameanza kutawala  kutokana sheria za  Financial Fair Play  za UEFA,ndiyo maana klabu inataka kupunguza matumizi yake na kwa usemi huo,chelsea wanajiandaa kuwauza baadhi ya wachezaji wake 28 waliopo  kwa mkopo kwenye klabu mbambali ikiwa ni pamoja na Victor Moses.

Mikel amejikuta kwenye wakati mgumu tangu kuwasili kwa Matic kwa dau la £21 million mwezi January na Chelsea wanaimani kuwa atahitaji gharama kubwa kwa sababu bado anamkataba na timu hiyo wa miaka mitatu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!