Searching...
Image and video hosting by TinyPic
18 December 2014
Thursday, December 18, 2014

Kumbe Marco Reus naye ni tatizo?


Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Borussian Dortmund, Marco Reus amepigwa faini ya Euro 540,000 kutokan na kuendesha gari bila kuwa na Leseni. 

Marco Reus mwenye umri wa miaka 25 amekamatwa na Police na baada ya mahojiano ikabainika kuwa winga huyo hakuwa na leseni ya Udereva.

Akizungumza baada ya tukio hilo, Marco Reus amekiri kuwa alichofanya ni jambo la kitoto na hapaswi kurudia tena. Tangu mwaka 2011 hili ni kama tukio la tano kwa mchezaji huyo kukamatwa huku matukio mengine yakihusisha mwendo kasi ambao amekuwa akiendesha kinyume na taratibu.

Marco Reus ambeye alikosa fainali za kombe la Dunia kule Brazil kutokana na kuumia dakika za mwisho, msimu huu amekuwa akihusishwa na kutimka klabu hapo huku timu kubwa barani Ulaya zikipigana vikumbo kugombea saini yake.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!