Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 December 2014
Monday, December 01, 2014

Miezi miwili migumu zaidi kwa Southampton kuonyesha ubora wake EPL.



 Na Abuu Hussein, 
0715 765 848. 

Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, kumekuwapo na mapinduzi makubwa katika ramani ya mchezo wa soka kwa kuibuka timu mpya ambazo hapo awali hazikupewa nafasi ya kufanya vizuri na kuzibwaga timu kubwa.


Katika ligi inayofutiliwa zaidi na inayosemekani kuwa zaidi kuliko zote duniani ya Uingereza, kumekuwa na mtifuano mkubwa wa kugombea nafasi za juu katika ligi hiyo ili kujihakishia kuchukua ubingwa na kufuzu katika mashindano ya ulaya ambapo vigogo wa ligi hiyo Man U, Chelsea,Man City, Arsenal,Liverpool na Tottenham wamekuwa wakipambana kukaa nafasi za juu. 

Katika kile kisichotarajiwa kumeibuka timu ya Southampton inayotishia uhai wa moja ya timu kubwa kutofuzu katika michuano ya ulaya kutokana na kusakata kabumbu safi kabisa na kuibuka na matokeo ya ushindi huku wakijikusanyia pointi 26.

Pointi hizi zinawafanya kuzidiwa alama moja tu na  Manchester City wanaoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ya England na pointi 7 nyuma ya vinara Chelsea wenye pointi 33 huku wakiwatupa mbali Manchester United, Arsenal na Liverpool. 

Southampton inayofundishwa na kocha Mholanzi, Ronald Koeman inakabiliwa na ratiba ngumu katika kipindi cha miezi miwili yaani mwezi huu wa Desemba na Januari mwakani kwa kukabiliana na timu ngumu na zinazoifukuzia kwa karibu ambazo ni Arsenal na Manchester United.

Baada ya hapo, itapumzika mechi mbili kwa kucheza na Burnley, Shiffield United na timu nyingine ngumu Everton, Craystal palece kabla ya kuumaliza mwezi Desemba kwa kupambana na vinara wa ligi Chelsea. 

January mwakani Southampton wataanza kupambana na Arsenal, Manchester United na kumaliza na mpambano zidi ya Newcastal United.

Michezo hiyo itatoa taswira ya msimamo halisi wa “Big four” na kuona kama kweli Southampton wanaweza kuvunja ule utaratibu wa timu kubwa na zenye uwezo kifedha kumaliza katika nafasi nne za juu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!