Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 December 2014
Monday, December 01, 2014

Messi apigwa na chupa ya maji.


Na Chikoti Cico

Mchezaji wa timu ya Barcelona, Lionel Messi apigwa na chupa ya maji kwenye mchezo dhidi ya Valencia uliochezwa siku ya Jumapili kwenye uwanja wa Mestalla na kuisha kwa Barcelona kushinda kwa goli 1-0, goli lilifungwa na kiungo Sergio Busquets kwenye dakika ya 94 ya mchezo huo.

Wakati wachezaji wa Barcelona wakishangilia goli hilo karibu na kibendera cha kona karibu na wanapokaa mashabiki wa Valencia chupa ya maji iliyoonekana kurushwa uwanjani na kutua kichwani kwa Messi kitendo kilichosababisha mchezaji huyo kubaki ameshika kichwa kwa maumivu.

Mchezo huo uliokuwa wa kupiga ni kupige huku kila timu ikitafuta ushindi huku pia ukihusisha rafu za hapa na pale kutoka kwa timu zote mbili zilizopelekea kwa refa wa mchezo huo David Fernandez kuwaonyesha wachezaji nane kadi za njano.

Goli la Barcelona lilitokana na krosi safi ya Messi iliyounganishwa kwa kichwa na Neymar kabla ya kuokolewa na kipa wa Valencia Diego Alves na Sergio Busquets kumalizia mpira huo kuipatia goli la ushindi timu ya Barcelona.

Ushindi huo umeifanya Barcelona kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya Hispania maarufu kama la liga huku ikifikisha alama 31 ingawa bado wamepitwa na vinara wa ligi hiyo timu ya Real Madrid kwa alama mbili, Madrid wanaongoza ligi hiyo wakiwa na alama 33

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!