Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 December 2014
Saturday, December 06, 2014

Apewa mkataba baada ya kumkaba Messi


Na Chikoti Cico

Ni ngumu kuamini lakini ndicho kilichotokea kwa mchezaji wa Everton, Mohamed Besic ambaye kabla ya kujiunga na timu hiyo inayofundishwa na Kocha Roberto Matinez alikuwa anaichezea timu ya Ferencvaros ya Hangari.

Besic baada ya kumkaba Messi na kuonyesha kiwango bora kwenye mechi ya kombe la Dunia kati ya Argentina dhidi ya Bosnia, mchezo uliopigwa kwenye uwanja maarufu wa Maracana huku akishuhudiwa na Martinez ndipo kocha huyo alipoamua kutafuta saini ya Besic kutokea Ferencvaros.

Pamoja na kwamba Argentina walishinda kwa magoli 2-1 huku Messi akifunga goli moja, bado hilo halikumzuia Martinez kutokumsajili mchezaji huyo ambaye amecheza mechi zote za Everton tokea kuanza kwa msimu huu huku akianza kwenye kikosi cha kwanza katika mechi tatu zilizopita.

Martinez akimwongelea mchezaji huyo kutoka Bosnia na kwanini alimsajili kwa pauni milioni 4 alisema “alimkaba Messi vizuri kipindi cha kwanza, nilimjua mara ya kwanza akiwa kijana mdogo kule Hamburg, ni kijana mwenye uwezo bora”

Besic mwenye umri wa miaka 22 akielezea safari yake mpaka kufika Goodison Park alisema “ilikuwa ni hatua kubwa kwangu, kama nisingeondoka labda nisingekuwa nacheza hapa ningekuwa Uswisi kwenye klabu ya Basel.

Walikuwa na shauku ila baada ya kombe la Dunia, Everton walikuja na klabu kutoka Italia na Hispania pia”

Akiongelea kuhusu stori yake na kumkaba Messi huku akitabasamu Besic alisema “ ilikuwa vizuri, nilibadilishana jezi? Hapana hapana, mara zote huwa nabaki na jezi yangu, kuichezea Bosnia ni heshima kubwa”

Aliendela kusema “sina wa kumuiga, niliipenda Bayern Munich nilipokuwa mdogo walivyokuwa wanacheza, kamwe sijawahi kumshabikia mchezaji ama timu najua inaonekana ni ajabu ila ndivyo ilivyo”.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!