Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 December 2014
Saturday, December 06, 2014

Van Gaal uso kwa uso na adui yake.



Na Oscar Oscar Jr

Kocha wa Manchester United, Loius Van Gaal amekataa kuzungumzia uhusiano wake na Mdachi mwenzie kocha wa Southampton, Ronald Koeman. Makocha hao wamewahi kufanya kazi pamoja kwenye klabu ya Ajax kule nchini Uholanzi mwaka 2004.

Inadaiwa kuwa, makocha hao hawako kwenye mahusiano mazuri na wakiwa Ajax, Van Gaal alikuwa kocha mkuu huku Koeman akiwa kama mkurugenzi wa ufundi. Wawili hao wanakutana kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza siku ya Jumatatu kwenye dimba la St. Marrys.

Van Gaal amesema kuwa haoni umuhimu wa kuzungumzia uhusiano wake na Mdachi mwenzie kwa sababu anakwenda kucheza na timu na sio kocha wa Southampton. 

Southampton ambao wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi 26, wametoka kupoteza mechi mbili mfululizo huku United wao wakizinduka na kufufua matumaini ya kufanya vizuri kwa kushinda mara nne mfululizo.

Southampton ambao msimu uliopita walimaliza kwenye nafasi ya nane, msimu huu pamoja na kufanya vema kwenye michezo yao ya awali bado wameshindwa kutamba wanapocheza na timu ambao zilimaliza kwenye nafasi saba za juu msimu uliopita.

Hivi karibuni wametoka kufungwa na bingwa mtetezi, Manchester City na Arsenal ambao walimaliza nafasi ya nne. Msimu huu pia, wameshindwa kutamba walipocheza na Liverpool, Spurs na Chelsea.

Mechi hiyo ya siku ya Jumatatu usiku, inatarajiwa kuleta upinzani mkubwa hasa ukizingatia kuwa, Manchester United wanapigana kuhakikisha wanamaliza kwenye moja ya nafasi nne za juu huku majeruhi nayo yakizidi kuwaandama.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!