Searching...
Image and video hosting by TinyPic
17 November 2014
Monday, November 17, 2014

Yohan Cabaye sasa ni Anfield au Emirates.

Na Oscar Oscar Jr

Kocha mpya wa Inter Millan, ameamua kuvamia sasa kwenye ligi kuu ya Uingereza na kuchukuwa majembe ambayo anadhani, yanauwezo wa kuirejesha timu hiyo kwenye ubora wake. 

Joe Campbell wa Arsenal, Erik Lamela wa Tottenham HotSpurs, Fabio Borini wa Liverpool, Alexander Kolarov wa Manchester City wanatajwa kuwa kwenye orodha ya kocha huyo huku, Mancini akijiandaa kumtwaa Mkongwe Steven Gerrard na kumpa nafasi kwenye kikosi chake.

Southampton ambao wanaonekana kufanya vizuri kwenye ligi kuu nchini Uingereza ambapo mpaka sasa wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 25, wanajiandaa kumnasa beki matata wa Uholanzi na klabu ya Porto, Bruno Martins Indi.

Southampton wanadaiwa kupata upinzani kutoka kwa klabu ya Manchester United ambao nao wanatajwa kuuwinda mchezaji huyo ambaye ni mwezi wa saba tu alipojiunga na Porto akitokea kwenye klabu ya Fayenoord ya nchini Uholanzi.

Kiungo wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya PSG, Yohan Cabaye anatajwa kutokuwa na furaha kwenye kikosi hicho na tayari kuna habari za kurejea tena kwenye ligi ku ya Uingereza. 

Timu ambazo zinatajwa kumuwania mchezaji huyo ni Liverpool na Arsenal ambao wote wanaonekana kuwa na mapungufu kwenye eneo la kiungo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!