Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 November 2014
Friday, November 21, 2014

Welbeck na Walcott kuwakosa Man United.


Na Oscar Oscar Jr

Mshambuliaji wa Arsenal, Theo Walcott atakuwa nje kwenye mpambano kati ya Arsenal dhidi ya Manchester United mchezo unaotarajiwa kupigwa siku ya Jumamosi majira ya saa 2:30 Usiku kwa saa za Afrika mashariki ndani ya dimba la Emirates.

Walcott ambaye aliumia kwenye mchezo wa kombe la FA kwenye mechi dhidi ya Tottenham Hotspurs msimu uliopita, anatarajiwa kuwa nje ya kikosi cha kocha Wenger ambaye hataki kumuharakisha dimbani. 

Tayari Walcott amecheza mechi mbili tangu arejee kutoka majeruhi lakini, mechi zote aliingia kama mchezaji wa akiba.

Habari njema kwa Gunners, ni kurejea kwenye kikosi hicho kwa mshambuliaji Olivier Giroud ambaye alikuwa nje baada ya kuumia mguu kwenye mechi yao dhidi ya Everton mapema msimu huu. 

Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Danny Welbeck ambaye ameonekana kuwa kwenye kiwango kizuri baada ya kutua Arsenal, huenda akaukosa pia mchezo huo kutokana na kupata majeraha kidogo mazoezini.

Naye kocha wa Manchester United, Loius Van Gaal hakusita kusema kuwa, Welbeck ameimarika sana ndani ya miezi ya hivi karibuni kutokana na kupata nafasi ya kucheza kama mshambuliaji wa kati. Welbeck atasubiri ripoti ya daktari ili kujuwa kama atakuwa sehemu ya kikosi cha Arsenal hapo kesho.

Van Gaal amesema kuwa, isingekuwa rahisi kwa mchezaji huyo kucheza kama mshambuliaji pekee akiwa Manchester kwa sababu kuna Rooney na Roben Van Persie hivyo, kuondoka ni chaguo sahihi kwa Welbeck.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!