Na Chikoti Cico
Baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Moscow kati ya CSKA Moscow dhidi ya Manchester City kuisha kwa sare ya magoli 2-2, timu hizo zinarudiana tena kwenye mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa ligi ya mabingwa Ulaya jijini Manchester kwenye uwanja wa Etihad.
Manchester City wanaingia kwenye mchezo huo wakihitaji ushindi tu ili kufufua matumaini ya kuvuka hatua ya makundi kwani mpaka sasa wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi E huku wakiwa na alama mbili kati ya michezo mitatu ya mzunguko wa kwanza.
Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini atawakosa viungo Frank Lampard, David Silva na beki wa kushoto, Aleksandar Kolarov ambao ni majeruhi akitegemea ushindi wa bao 1-0 aliopata dhidi ya Manchester United kwenye ligi kuu ya Uingereza, utaamsha ari na hamasa kwa wachezaji wake ili kuweza kupata matokeo mazuri dhidi ya CSKA Moscow.
Kikosi cha Manchester City kinaweza kuwa hivi: Hart; Clichy, Kompany, Demichelis, Zabaleta; Fernando, Toure, Nasri, Milner; Dzeko, Aguero
Nayo timu ya CSKA Moscow inatarajia kuingia kwenye mchezo huo kutafuta ushindi kwani ili kufufua matumaini ya kupata nafasi ya Europa na labda kuingia hatua ya makundi.
Mpaka sasa wanashika mkia kwenye msimamo wa kundi E huku wakiwa na alama moja kati ya michezo mitatu ya mzunguko wa kwanza wa ligi ya mabingwa Ulaya.
CSKA Moscow inayofundishwa na kocha Leonid Viktorovich Slutsky, itawakosa kiungo Rasmus Elm na mshambuliaji Kirill Panchenko ambao ni majeruhi.
Wakati huo huo, kocha Leonid atamtegemea zaidi mshambuliaji kutoka Nigeria Ahmed Musa kuongoza safu ya ushambuliaji ya Moscow.
Kikosi cha CSKA Moscow kinaweza kuwa hivi: Akinfeev; V Berezutski, Ignashevich, A Berezutski, Schennikov, Fernandes; Eremenko, Natcho, Tosic; Musa, Doumbia
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.