Searching...
Image and video hosting by TinyPic
5 November 2014
Wednesday, November 05, 2014

Uchambuzi: Ajax vs Barcelona


Na Chikoti Cico

Ligi ya mabingwa Ulaya inatarajiwa kuendelea tena leo na moja ya mechi itakayopigwa usiku huu ni kati ya Ajax dhidi ya Barcelona mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Amsterdam Arena nchini Uholanzi. Kwenye mechi ya kwanza iliyopigwa Nou camp Barcelona walishinda kwa magoli 3-1.

Ajax inayofundishwa na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi Frank de Boer inahitajika kupigana inavyowezekana kupata matokeo mazuri nyumbani ili kufufua matumaini ya kuvuka hatua ya makundi kwani mpaka sasa wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi F wakiwa na alama mbili tu kati ya mechi tatu walizocheza kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi ya mabingwa Ulaya.

Kuelekea kwenye mchezo huo Ajax watamkosa kiungo Victor Fuscher ambae ni majeruhi, wakati huo takwimu zinaonyesha Ajax wamekuwa na rekodi nzuri nyumbani dhidi ya timu za Hispania kwani katika michezo 17 waliyocheza wameweza kushinda michezo tisa.

Kikosi cha Ajax kinaweza kuwa hivi: Cillessen; Van Rhijn, Moisander, Veltman, Viergever; Andersen, Klaassen, Zimling; Schone, Sigthorsson, Milik

Barcelona ambao wamekuwa na matokeo mabaya kwenye mechi zilizopita za la liga baada ya kufungwa na Real Madrid na Celta Vigo hivyo kupoteza alama sita na kushushwa mpaka nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, wanaweza kuvuka hatua ya makundi kama watashinda mchezo dhidi ya Ajax na Apole ikishindwa kumfunga PSG kwenye mchezo mwingine wa kundi F.

Wakishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi F wakiwa na alama sita Barcelona inayofundishwa na kocha Luis Enrique itawategemea zaidi washambuliaji Lionel Messi, Neymar na Suarez kutafuta alama tatu muhimu huku ikitarajiwa kuwakosa mabeki Jeremy Mathieu na Thomas Vermalen ambao ni majeruhi huku kiungo Andres Iniesta akiwa na hatihati ya kutokucheza mchezo huo.

Kwa upande wa Luis Suarez ni kama anarejea nyumbani kwani aliwashawai kuichezea Ajax kwa miaka mitatu na nusu kabla ya kusajiliwa na Liverpool mwaka 2011 na baadaye kuhamia Barcelona ingawa leo atatamani kuwafunga Ajax na kuipa ushindi Barcelona.

Kikosi cha Barcelona kinaweza kuwa hivi: Ter Stegen; Alves, Mascherano, Piqué, Adriano/Alda; Busquets, Rakitic, Xavi; Luis Suárez, Messi, Neymar.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!