Na Chikoti Cico
Mwaka
1998 timu ya Inter Milan ilicheza na Lazio kwenye fainali ya kombe la
UEFA (UEFA CUP) mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Parc des Princes
jijini Paris, Milan ilishinda mchezo huo kwa magoli 3-0 huku Ronaldo de
Lima akitupia goli la tatu mbele ya beki mahiri wa Lazio kipindi hicho
Alessandro Nesta.
Baada ya mchezo huo wa fainali wakati flani Alessandro Nesta akihojiwa na waandishi wa habari aliulizwa swali kwamba “ni mshambuliaji gani hatari zaidi umewahi kukutana nae” akijibu swali hilo Nesta alisema “ uzoefu mbaya nIliokuwa nao ni kucheza dhidi ya Ronaldo tulipokutana na Inter Milan mwaka 1998 kwenye fainali ya kombe la UEFA Paris”
“Ni mchezaji bora, nimetazama video ya mchezo ule mara nyingi toka wakati huo kuangalia wapi nilifanya kosa, tulifungwa 3-0 lakini sifikiri kama yalikuwa makosa yangu, Ronaldo hazuiliki, ana kasi sana anafanya wengine wote waonekane kama wamesimama wima”. Hayo ni maneno ya Nesta akimwelezea Ronaldo de Lima.
Nimeamua kuanza na kisa hicho kidogo kuonyesha ni kwa jinsi gani Ronaldo de Lima alikuwa ni hatari, huku akiwa amezaliwa nchini Brazili kwenye bara la America ya kusini.
Ronaldo hakika alikuwa ni mshambuliaji hatari kuwahi kutokea duniani mpaka kupachikwa jina la “el fenomeno”
Baada ya Ronaldo kustaafu soka, washambuliaji mbalimbali kutoka America ya Kusini wameendelea kuwika kwenye ligi mbalimbali duniani ingawa hawajaweza kufikia makali ya “el fenomeno” lakini wanajitahidi kuonyesha ubora wao na ni kama wanataka kuiambia dunia ya soka kwamba “sisi ni wadogo zake Ronaldo”
Katika ligi kuu nchini Uingereza washambuliaji kutoka America ya Kusini ambao waliwika na wanaendelea kuwika ni Luis Suarez, Sergio Aguero na Diego Costa nimetaja kwa uchache tu.
Suarez ambaye kwasasa anachezea timu ya Barcelona aliweza kuonyesha ubora wake kwenye ligi kuu ya nchini Uingereza na mpaka kuibuka mfungaji bora na kunyakua kiatu cha dhahabu huku akifunga jumla ya magoli 33 kwenye msimu wa 2013/2014.
Pamoja na kashfa mbalimbali zilizomkumba akiwa Liverpool, bado Suarez aliweza kuuthibitishia ulimwengu wa soka kwamba anatoka bara moja na Ronaldo de Lima kwa kufunga magoli muhimu na yenye ubora na hatimaye kuibuka mfungaji bora wa ligi hiyo.
Wakati Luis Suarez ananyakua tuzo ya ufungaji bora nyuma yake, alikuwa anakimbizana na mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero.
Baada ya kuwika sana akiwa na timu ya Atletico Madrid, Aguero alisajiliwa na City mwaka 2011 na msimu wake wa kwanza tu aliweza kufunga magoli 23 kati ya mechi 34 alizocheza.
Aguero ambaye anatoka nchini Argentina naye pia ameonyesha dhahiri kwamba ni mmoja wa wadogo zake Ronaldo de Lima kwani mpaka sasa, anaongoza kwenye listi ya wafungaji nchini Uingereza huku akiwa ameshafunga magoli 10 kati ya mechi 10 alizocheza toka msimu wa ligi wa 2014/15 kuanza.
Anayemfuatia Aguero kwenye listi ya wafungaji, ni mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Hispania Diego Costa. Huyu pia ni mzaliwa wa Bara la America ya Kusini akizaliwa nchini Brazili lakini akaamua kuchukua uraia wa Hispania hivyo bado ni mdogo wake Ronaldo ambaye nae anafanya vyema katika ufungaji wa magoli.
Ukiwa ni msimu wake wa kwanza kuichezea Chelsea baada ya kusajiliwa kutoka Atletico Madrid, Costa mpaka sasa ana magoli tisa kati ya mechi nane alizoichezea Chelsea toka kuanza kwa ligi kuu nchini Uingereza.
Pamoja na kusumbuliwa na majeruhi, bado Costa ameonyesha ni jinsi gani ana unasaba na “el fenomeno” katika ufungaji wa magoli.
Ni mapema kusema ila yawezekana mbio za kuwania kiatu cha dhahabu kwa msimu huu wa mwaka 2014/2015 kwenye ligi kuu ya nchini Uingereza, zikawahusisha wadogo zake Ronaldo LuÃs Nazário de Lima maarufu kama “el fenomeno”.
NAWASILISHA

0 comments:
Post a Comment