Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 November 2014
Monday, November 03, 2014

Uchambuzi: Arsenal vs Anderlecht


Na Chikoti Chiko

Baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza, Ligi ya mabingwa Ulaya itaendelea tena wiki hii kwa mechi za kwanza za mzunguko wa pili na moja mechi hizo ni kati ya Arsenal dhidi ya Anderlecht, mchezo utakaopigwa siku ya Jumanne saa 4:45 usiku kwa saa za Afrika Mashariki kwenye uwanja wa Emirates jijini London.

Timu ya Arsenal inayofundishwa na kocha Arsene Wenger inatarajiwa kuingia kwenye mchezo dhidi ya Anderlecht kutafuta alama tatu muhimu ambazo zinaweza kuwavusha hatua ya makundi, mpaka sasa timu ya Arsenal inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi D wakiwa na alama sita kati ya mechi tatu walizocheza za mzunguko wa kwanza.

Katika kutafuta alama hizo tatu muhimu kwenye mchezo huo kocha Wenger ataendelea kuwakosa Mesut Ozil, Olivier Giroud, David Ospina, Mathieu Debuchy na Laurent Koscienly ambao bado ni majeruhi.

Wakati huo huo kureja kwa winga Theo Walcott kutaiongezea makali timu ya Arsenal huku kipa Wojciech Szczesny akirejea golini baada ya kukosa mchezo wa kwanza wakati akitumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Kikosi cha Arsenal kinaweza kuwa hivi: Szczesny; Chambers, Mertesacker, Monreal, Gibbs; Arteta, Wilshere, Ramsey; Cazorla, Sanchez, Welbeck

Timu ya Anderlecht baada ya kupoteza mchezo wa kwanza nyumbani Brussels, Ubelgiji kwa kufungwa magoli 2-1 na Arsenal wanatarajiwa kuingia kwenye mchezo wa Jumanne wakitaka kulipa kisasi lakini pia kutafuta alama tatu muhimu ili kufufua matumaini ya kuvuka hatua ya makundi hasa baada ya kupoteza michezo miwili na kutoka sare mchezo mmoja kwenye mzunguko wa kwanza hivyo kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi D wakiwa na alama moja.

Kocha wa Anderlecht Besnik Hasi anatarajia kumkosa beki Fabrice N’Sakala aliye majeruhi huku pia beki mwingine Bram Nuytinck akiwa na hatihati ya kutokucheza kwenye mchezo huo dhidi ya Arsenal kutokana na kuwa majeruhi.

Kikosi cha Anderlecht kinaweza kuwa hivi: Proto; Vanden Borre, Mbemba, Heylen, Deschacht; Defour, Tielemans; Najar, Praet, Suarez; Mitrovic

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!