Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 November 2014
Friday, November 07, 2014

Tetesi za Usajili za Arsenal




Na Oscar Oscar Jr

Kabla ya Danny Welbeck kusajiliwa na kocha wa Arsenal, Mfaransa Arsene Wenger kulikuwa na taarifa za kocha huyo kumuhitaji beki wa kati ya timu hiyo wa Manchester United, Chris Smalling. 

Wenger anaonekana kuwa shabiki mkubwa wa Smalling na kutokana na majeruhi ya beki Laurent Conscienly na Methieu Debuchy, tayari amewatuma mascout kutafuta beki wa kuziba nafasi hiyo.

Kiungo wa klabu ya Paris Saint German, Adrien Rabiot, 19, alikuwa kwenye rada za kutua mwezi January kwenye dimba la Emirates lakini dili limekwama baada ya kiungo huyo kusaini mkataba mpya na wababe hao wa nchini Ufaransa.

Rada za kusaki kiungo kwa sasa, zimehamia klabu ya Southampton ambapo, Morgan Schneiderlin ameendelea kutajwa kama mtu wa kuja kuimarisha safu ya kiungo ya timu hiyo.
 
Katika magazeti ya leo barani Ulaya, beki wa Celtic, Virgil van Dijk na Ron Vlaar wa Aston Villa, bado wameendelea kuwekwa kwenye orodha ya walinzi wa kati wanaohitajika na kocha Wenger. 

Katika habari za kushitukiza, klabu ya Fiorentina imejitokeza na kutaka kumchukuwa kwa mkopo kiungo mshambuliaji wa Arsenal, Theo Walcott.

Fiorentina wanadai, wanataka kumpatia winga huyo nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza kwa sababu, bado hajaweza kupata nafasi hiyo tangu arejee kutoka majeruhi. 

Bado ni vigumu sana kujua ni kipi Arsenal wataamua juu ya Theo Walcott kwani kuna mazungumzo ya kumuongeza mshambuliaji huyo mkataba mpya ambayo yanaendelea. 

Arsenal kwa sasa wanashika nafasi ya nne wakiwa na pointi 17 kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza nyuma ya Manchester City wenye pointi 20, Southampton wenye pointi 22 na vinara Chelsea wenye pointi 26.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!