Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 November 2014
Friday, November 07, 2014

Tetesi za Usajili wa Manchester United


Na Oscar Oscar Jr

Klabu ya Manchester United imeendelea kuhusishwa na wachezaji kadhaa huku Kipa wake namba moja kwa sasa, David De Gea  akiendelea kuhusishwa na Mabingwa wa Ulaya, klabu ya Real Madrid. Winga wa West Bromwich Albion, mzaliwa wa Burundi Saido Berahino ametajwa kutua Old Trafford.

Berahino tayari amefunga magoli saba ya ligi kuu Uingereza na tayari klabu za Liverpool, Tottenham HotSpurs na Manchester United zikitajwa kupigana vikumbo ili kumnasa mshambuliaji huyo. 

Berahino ni shabiki mkubwa wa Manchester United lakini inaelezwa kuwa, mama yake anayejulikana kwa jina la Liliane, ni mnazi wa kutupwa wa klabu ya Arsenal.

Tofauti hiyo, inadaiwa kupunguza uwezekano wa Spurs kuweza kumnasa mchezaji huo kwa sababu ya upinzani mkali uliopo kati ya timu anayoshabikia mama yake Berahino (Arsenal) na Spurs. 

Fabio Coetrao anatajwa kuwaniwa na Manchester United kutoka katika klabu ya Real Madrid lakini, kuna uwezekano dili hilo likahusishwa na David De Gea kuelekea Real Madrid.

Kwa upande wa pili, makosa aliyofanya kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson ya kumuuza kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Paul Pogba kwenda Juventus, yanaweza kuwanufaisha wapinzani wao klabu ya Manchester City. 

Taarifa zinadai kuwa, Manchester City watamuuza Yaya Toure mwishoni mwa msimu na watu wanaotajwa kuziba nafasi yake ni Ross Barkley kutoka Everton na Paul Pogba wa Juventus.

Manchester United kwa sasa, wako kwenye nafasi ya 10 huku wakiwa wamefunga mabao 16 msimu huu. Jumamosi hii watakuwa wenyeji wa timu ya Crystal Place kwenye dimba la Old Trafford wakisaka alama tatu muhimu baada ya wiki iliyopita kupigwa na Manchester City bao 1-0.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!