Mourinho amtikisa Roberto Di Mateo
Na Oscar Oscar Jr
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho ameibuka na kudai kuwa kupata ubingwa wa michuano ya Klabu bingwa Ulaya wakati mwingine sio kipimo kilichotukuka kwa kocha.
Mourinho ameyasema hayo kuelekea mchezo wao dhdi ya timu ya Schalke 04 ya nchini Ujerumani ambayo kwa sasa inanolewa na kocha wa zamani wa Chelsea, Roberto Di Mateo.
Di Mateo atakumbukwa na mashabiki wengi wa Chelsea hasa baada ya kuwafanya kutwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 2012 mbele ya wababe wa Ujerumani, timu ya Bayern Munich.
Mourinho amesema, timu kama Chelsea na Liverpool zimewahi kutwaa taji hilo huku zikimaliza ligi nafasi ya sita, hivyo hadhani kama kutwaa taji hilo ndiyo kipimo ya kuonyesha ubora wa kocha.
Akiulizwa juu ya historia iliyowekwa na kocha Di Mateo kwa kuipatia timu hiyo kombe la klabu bingwa Ulaya, Mourinho alisema kuwa, kila mtu anahistoria yake pale Chelsea.
Timu kama Chelsea inawatu wa kila aina walioweka historia kuanzia wachezaji hadi makocha kwa hiyo, kila mtu anafanya jambo lake kwa wakati wake.
Mourinho ambaye amewahi kutwaa taji hilo mara mbili huku akiviongoza vilabu vya Porto na Inter Millan, ameendelea kusisitiza kuwa, lengo la Chelsea ni kupata ushindi ili kujihakikishia nafasi ya uongozi wa kundi.
Kocha huyo anatarajia kuanzisha kikosi imara kuelekea mchezo wa leo Usiku pale watakapo vaana na timu hiyo kutoka Ujerumani. Chelsea ambayo inaongoza ligi kuu ya Uingereza, inaonekana moto wa kuotea mbali huku wachezaji waliosajili msimu huu, wakiongezea kikosi hicho ubora. Diego Costa, Thibout Courtois na Cesc Fabregas wote wanatarajia kuanza kwenye mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment