Searching...
Image and video hosting by TinyPic
17 August 2014
Sunday, August 17, 2014

Loius Van Gaal akubali lawama



Na Oscar Oscar Jr

Akiwa amebeba matumaini makubwa sana ya mashabiki wa Man United kocha Loius Van Gaal alijikuta akipoteza mchezo wake wa kwanza ndani ya dimba la Old Trafford mbele ya timu ya Swansea City.

Louis van Gaal alikubali lawama baada ya Manchester United kulazwa 2-1 nyumbani na Swansea City Jumamosi kwenye mechi yake ya kwanza Ligi ya Premia akiwa meneja. 

Van Gaal alipanga timu yake kwa muundo wa 3-4-1-2 alioanza kuutumia wakati wa kujiandaa kwa ligi na kufanikiwa, lakini bao la Ki lilimlazimisha kubadilisha kipindi cha pili. 

 Majeraha yalimlazimisha Van Gaal kuchezesha chipukizi Tyler Blackett na Jesse Lingard mechi zao za kwanza, lakini alipuuzia mbali mapendekezo kwamba matokeo hayo huenda yakamfanya kununua wachezaji upesi sokoni. 

Mholanzi huyo wa miaka 63 anajaribu kukwamua United baada yao kumaliza nambari saba msimu uliopita, lakini enzi yake ilianza vibaya pale Swansea walipojipatia ushindi wao wa kwanza kabisa ligini Old Trafford. 

Ki Sung-yueng aliweka Swansea kifua mbele dakika ya 28 na ingawa nahodha mpya wa United Wayne Rooney aliwasawazishia dakika ya 53, Gylfi Sigurdsson aliipa timu hiyo ya Wales ushindi zikiwa zimesalia dakika 18 za kucheza. 

Majeraha yalimlazimisha Van Gaal kuchezesha chipukizi Tyler Blackett na Jesse Lingard mechi zao za kwanza, lakini alipuuzilia mbali mapendekezo kwamba matokeo hayo huenda yakamfanya kununua wachezaji upesi sokoni. 

Baada ya kupoteza mchezo huo, kocha huyo alidai "Tulikuwa na wasiwasi sana kipindi cha kwanza, na tulifanya maamuzi mabaya na tunajuta. Kipindi cha pili, hatukucheza kama timu. Kwa hivyo, ni mimi ninayefaa kulaumiwa,” akasema Van Gaal.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!